Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Rois 21.18
Bible en Swahili de l’est


1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba.Esaïe 62.4 Matthieu 1.10 1 Chroniques 3.13 2 Rois 20.21 2 Chroniques 32.33-33.9
2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli.2 Chroniques 36.14 2 Rois 16.2-16.4 2 Rois 22.17 2 Rois 21.7 Deutéronome 12.31
3 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.2 Rois 18.4 2 Rois 17.16 Deutéronome 17.3 Deutéronome 4.19 1 Rois 16.31-16.33
4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu.2 Samuel 7.13 1 Rois 8.29 Jérémie 32.34 2 Rois 16.10-16.16 1 Rois 9.3
5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana.1 Rois 7.12 2 Rois 23.4 2 Rois 23.12 1 Rois 6.36 Ezéchiel 40.32
6 Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.Lévitique 18.21 Lévitique 19.31 2 Rois 17.17 2 Rois 16.3 Lévitique 19.26
7 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;1 Rois 9.3 1 Rois 8.29 2 Chroniques 7.16 2 Rois 23.27 2 Rois 21.4
8 wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa.2 Samuel 7.10 Lévitique 26.3-26.13 Deutéronome 5.28-5.29 Jérémie 7.3-7.7 Jérémie 17.20-17.27
9 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.Proverbes 29.12 Daniel 9.6 Daniel 9.10-9.11 Néhémie 9.29-9.30 Jacques 4.17
10 Bwana akanena kwa watumishi wake manabii, akisema,Néhémie 9.30 Matthieu 23.34-23.37 2 Chroniques 36.15 2 Chroniques 33.10 Néhémie 9.26
11 Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya machukizo haya, na kutenda vibaya kuliko yote waliyoyatenda Waamori, waliokuwa kabla yake, naye akawakosesha Yuda kwa sanamu zake;2 Rois 24.3-24.4 1 Rois 21.26 2 Rois 21.9 Jérémie 15.4 2 Rois 21.21
12 kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili.Jérémie 19.3 1 Samuel 3.11 Amos 3.2 2 Rois 22.16 Michée 3.12
13 Nami nitanyosha juu ya Yerusalemu kamba ya Samaria, na timazi ya nyumba ya Ahabu; nami nitaifuta Yerusalemu, kama mtu afutavyo sahani, kuifuta na kuifudikiza.Esaïe 34.11 Lamentations 2.8 Amos 7.7-7.8 Jérémie 25.9 Ezéchiel 23.31-23.34
14 Nami nitawatupa mabaki ya urithi wangu, na kuwatia mikononi mwa adui zao; nao watakuwa nyara na mateka kwa adui zao wote;Jérémie 23.33 Psaumes 89.38-89.45 2 Rois 19.4 Lamentations 5.20 Psaumes 106.40-106.43
15 kwa sababu wametenda yaliyo mabaya machoni pangu, na kunikasirisha, tangu siku ile walipotoka baba zao katika Misri, hata leo hivi.Ezéchiel 20.21 Psaumes 106.34-106.40 Deutéronome 9.21 Ezéchiel 23.3 Ezéchiel 20.4
16 Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa Bwana.2 Rois 21.11 2 Rois 24.3-24.4 Matthieu 27.6 2 Chroniques 33.9 Jérémie 15.4
17 Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na kosa lake alilolikosa, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?2 Chroniques 33.1-33.20 2 Rois 20.20-20.21
18 Manase akalala na babaze, akazikwa katika bustani ya nyumba yake mwenyewe, yaani, bustani ya Uza. Na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.2 Chroniques 33.20 2 Rois 21.26 2 Chroniques 21.20 2 Chroniques 32.33 2 Chroniques 24.25
19 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka miwili huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Meshulemethi, binti Haruzi wa Yotba.2 Chroniques 33.21-33.23 1 Rois 22.51 2 Rois 15.23 1 Rois 15.25 Matthieu 1.10
20 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kama Manase babaye alivyofanya.2 Rois 21.11 2 Chroniques 33.22-33.23 Actes 7.51 Nombres 32.14 2 Rois 21.2-21.7
21 Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu. 22 Akamwacha Bwana, Mungu wa babaze, wala hakuiendea njia ya Bwana.2 Rois 22.17 1 Rois 11.33 1 Chroniques 28.9 Deutéronome 32.15 Jérémie 2.13
23 Nao watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, wakamwua mfalme ndani ya nyumba yake mwenyewe.2 Rois 12.20 2 Chroniques 33.24-33.25 2 Rois 14.19 1 Rois 16.9 1 Rois 15.27
24 Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya fitina juu yake mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake.2 Rois 14.5 1 Rois 12.20 1 Rois 12.1 1 Samuel 11.15 2 Rois 11.17
25 Basi mambo yote ya Amoni yaliyosalia, aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?2 Rois 20.20 2 Rois 21.17
26 Akazikwa kaburini mwake katika bustani ya Uza. Na Yosia mwanawe akatawala mahali pake.2 Rois 21.18 1 Rois 13.5 Matthieu 1.10

Cette Bible est dans le domaine public.