Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
2 Rois 7.9 Bible en Swahili de l’est
1 Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. Josué 3.5 1 Samuel 11.9 Ezéchiel 37.4 Exode 14.13 Exode 9.5-9.6 2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 2 Rois 5.18 Genèse 7.11 Malachie 3.10 Genèse 18.12-18.14 Romains 3.3 3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? Nombres 5.2-5.4 Nombres 12.14 Jérémie 8.14 Jérémie 27.13 Lévitique 13.45-13.46 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 2 Samuel 14.14 Hébreux 9.27 Esther 4.16 1 Chroniques 12.19 Luc 15.17-15.19 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 1 Samuel 30.17 Lévitique 27.26 Lévitique 27.8 Deutéronome 32.25 Ezéchiel 12.12 6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 2 Samuel 5.24 1 Rois 10.29 Job 15.21 Esaïe 36.9 2 Chroniques 12.2-12.3 7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. Psaumes 48.4-48.6 Proverbes 28.1 Job 18.11 Proverbes 21.1 Esaïe 2.20 8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. Josué 7.21 Jérémie 41.8 Matthieu 25.18 Matthieu 13.44 2 Rois 5.24 9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 2 Rois 7.3 Aggée 1.4-1.5 Philippiens 2.4 Nahum 1.15 2 Rois 7.6 10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. Marc 13.34-13.35 2 Rois 7.6-7.7 2 Samuel 18.26 2 Rois 7.11 Psaumes 127.1 11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. 12 Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini. 2 Rois 6.25-6.29 Josué 8.4 13 Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone. 2 Rois 7.4 Jérémie 14.18 2 Rois 6.33 Lamentations 4.9 2 Rois 5.13 14 Basi wakatwaa magari mawili na farasi zake; mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni, mkaangalie. 15 Wakawafuata mpaka Yordani; na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo, walivyovitupa Washami, wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme. Hébreux 12.1 Matthieu 16.26 Esaïe 22.24 Esaïe 31.7 Ezéchiel 18.31 16 Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana. 2 Rois 7.1 Esaïe 33.23 Esaïe 33.4 Nombres 23.19 2 Chroniques 14.12-14.15 17 Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia. 2 Rois 6.32 2 Rois 7.2 Hébreux 10.29 Juges 20.43 2 Rois 9.33 18 Ikatukia kama vile yule mtu wa Mungu alivyomwambia mfalme, Vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli, ndivyo vitakavyokuwa kesho, panapo saa hii, katika lango la Samaria; 2 Rois 7.1-7.2 2 Rois 6.32 Genèse 18.14 19 na yule akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 2 Rois 7.2 20 Ikampata vivyo hivyo, kwa kuwa watu wakamkanyaga langoni, akafa. Hébreux 3.18-3.19 Jérémie 17.5-17.6 Job 20.23 2 Chroniques 20.20 Esaïe 7.9