Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 116.15
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. 2 Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. 3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; 4 Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. 5 Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. 6 Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa. 7 Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu. 8 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka. 9 Nitaenenda mbele za Bwana Katika nchi za walio hai. 10 Naliamini, kwa maana nitasema, Mimi naliteswa sana. 11 Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo. 12 Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? 13 Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana; 14 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote. 15 Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake. 16 Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu. 17 Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana; 18 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote. 19 Katika nyua za nyumba ya Bwana, Ndani yako, Ee Yerusalemu.

Cette Bible est dans le domaine public.