Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 143.1 Bible en Swahili de l’est
Prière pour la délivrance
1 Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako. 2 Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki. 3 Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani. 4 Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. 5 Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. 6 Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. 7 Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni 8 Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. 9 Ee Bwana, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. 10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, 11 Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; 12 Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.