Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 143.3 Bible en Swahili de l’est
1 Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako. 2 Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.3 Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.4 Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. 5 Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. 6 Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. 7 Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni 8 Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. 9 Ee Bwana, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. 10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, 11 Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; 12 Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.