Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 21
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. Psaumes 28.7 Psaumes 63.11 Psaumes 62.7 Matthieu 2.2 Psaumes 99.4
2 Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. Psaumes 20.4-20.5 Psaumes 37.4 Psaumes 92.11 Hébreux 7.25 Psaumes 2.8-2.9
3 Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. 2 Samuel 12.30 1 Chroniques 20.2 2 Samuel 5.3 Ephésiens 1.3 Psaumes 31.19
4 Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. Psaumes 91.16 Psaumes 61.5-61.6 Psaumes 119.77 Psaumes 72.17 Psaumes 89.29
5 Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake. Psaumes 110.1 1 Chroniques 17.27 Ephésiens 1.20-1.22 Psaumes 62.7 Jean 17.1
6 Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. Psaumes 45.7 Psaumes 16.11 Galates 3.14 Luc 2.10-2.11 Actes 3.26
7 Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. Psaumes 16.8 Deutéronome 32.8-32.9 Psaumes 91.2 Psaumes 13.5 Psaumes 91.9-91.10
8 Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Esaïe 10.10 Psaumes 110.1-110.2 1 Samuel 31.3 Psaumes 2.9 Psaumes 72.9
9 Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala. Malachie 4.1 Lamentations 2.2 Esaïe 26.11 Psaumes 18.8 Psaumes 50.3
10 Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu. Psaumes 37.28 1 Rois 13.34 Esaïe 14.20 Psaumes 109.13 Job 18.16-18.19
11 Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza. Psaumes 10.2 Psaumes 2.1 Jérémie 11.18-11.19 Matthieu 2.8 Actes 4.17-4.18
12 Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale. Psaumes 7.12-7.13 Psaumes 18.40 Psaumes 56.9 Psaumes 9.3 Job 16.12-16.13
13 Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako. Apocalypse 19.1-19.6 Job 9.19 Psaumes 72.18-72.19 Psaumes 57.11 Psaumes 113.5

Cette Bible est dans le domaine public.