Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 63.6 Bible en Swahili de l’est
La soif de Dieu
1 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. 2 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. 3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. 4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu. 5 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. 6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. 7 Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. 8 Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza. 9 Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, Wataingia pande za nchi zilizo chini. 10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwa-mwitu. 11 Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.