Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 65.13 Bible en Swahili de l’est
Louange à Dieu pour ses bienfaits
1 Ee Mungu, sifa zakulaiki katika Sayuni, Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri. 2 Wewe usikiaye kuomba, Wote wenye mwili watakujia. 3 Ingawa maovu mengi yanamshinda, Wewe utayafunika maasi yetu. 4 Heri mtu yule umchaguaye, Na kumkaribisha akae nyuani mwako. Na tushibe wema wa nyumba yako, Patakatifu pa hekalu lako. 5 Kwa mambo ya kutisha utatujibu, Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu. Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia, Na la bahari iliyo mbali sana, 6 Milima waiweka imara kwa nguvu zako, Huku ukijifunga uweza kama mshipi. 7 Wautuliza uvumi wa bahari, Uvumi wa mawimbi yake, Na ghasia ya mataifa; 8 Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha. 9 Umeijilia nchi na kuisitawisha, Umeitajirisha sana; Mto wa Mungu umejaa maji; Wawaruzuku watu nafaka Maana ndiwe uitengenezaye ardhi. 10 Matuta yake wayajaza maji; Wapasawazisha palipoinuka, Wailainisha nchi kwa manyunyu; Waibariki mimea yake. 11 Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono. 12 Huyadondokea malisho ya nyikani, Na vilima vyajifunga furaha. 13 Na malisho yamevikwa kondoo, Na mabonde yamepambwa nafaka, Yanashangilia, naam, yanaimba.