14 Bwana akamwambia Musa, Moyo wa Farao ni mzito, anakataa kuwapa watu ruhusa waende zao. Exode 8.15 Exode 10.27 Exode 10.20 Exode 10.1 Esaïe 1.20 15 Mwendee Farao asubuhi; tazama, atoka kwenda majini; nawe simama karibu na ufuo wa mto ili upate kuonana naye; na ile fimbo iliyogeuzwa kuwa nyoka utaichukua mkononi mwako. Exode 8.20 Exode 2.5 Exode 7.10 Ezéchiel 29.3 Exode 4.2-4.4 16 Nawe umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, amenituma nije kwako, kusema, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia jangwani; nawe, tazama! Hujasikia hata sasa. Exode 3.18 Exode 9.1 Exode 3.12 Exode 9.13 Exode 8.1 17 Bwana asema, Katika jambo hili utanijua ya kuwa mimi ndimi Bwana; tazama, nitayapiga haya maji yaliyo mtoni kwa fimbo hii niliyo nayo mkononi mwangu, nayo yatageuzwa kuwa damu. Exode 4.9 Exode 5.2 Exode 7.5 Psaumes 9.16 Daniel 4.37 18 Na hao samaki walio mtoni watakufa, na huo mto utatoa uvundo; nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni. Exode 7.24 Exode 7.21 Nombres 21.5 Nombres 11.20 19 Bwana akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Shika fimbo yako, kaunyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya mito yao, juu ya vijito vyao, na juu ya maziwa ya maji yao, na juu ya visima vyao vyote vya maji, ili yageuke kuwa damu, nako kutakuwa na damu katika nchi yote ya Misri, katika vyombo vya mti, na katika vyombo vya jiwe. Exode 10.12 Exode 14.21 Exode 8.16 Exode 10.21 Exode 8.5-8.6 20 Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama Bwana alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu. Psaumes 78.44 Psaumes 105.29 Apocalypse 8.8 Nombres 20.8-20.12 Exode 7.17-7.18 21 Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote na Misri. Exode 7.18 Apocalypse 8.9 22 Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama Bwana alivyonena. Exode 7.11 2 Timothée 3.8 Exode 8.7-8.8 Jérémie 27.18 23 Farao akazunguka na kuingia nyumbani mwake, wala hata hilo hakuliweka moyoni. Habakuk 1.5 Job 7.17 Proverbes 22.17 Proverbes 24.32 Ezéchiel 40.4 24 Wamisri wote wakachimba-chimba kando ya mto ili wapate maji ya kunywa; maana, hawakuweza kuyanywa yale maji ya mtoni.