1 Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate.
Cantique 5.6 Cantique 1.7 Esaïe 26.9 Psaumes 63.6-63.8 Psaumes 130.1-130.2 2 Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. Romains 13.11 Matthieu 26.40-26.41 Cantique 5.5 Psaumes 22.1-22.2 Proverbes 8.2-8.3 3 Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
Cantique 5.7 Esaïe 21.11-21.12 Esaïe 21.6-21.8 Jean 20.15 Ezéchiel 3.17 4 Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.
Proverbes 8.17 Proverbes 4.13 Cantique 8.2 Esaïe 54.1-54.3 Osée 12.3-12.4 Le jeune homme 5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Cantique 2.7 Cantique 8.4 Michée 4.8 Les filles de Jérusalem 6 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
Cantique 8.5 Cantique 1.13 Cantique 4.6 Colossiens 3.1-3.2 Cantique 5.5 7 Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli.
Hébreux 1.14 1 Rois 9.22 2 Rois 6.17 1 Rois 14.27 1 Samuel 14.52 8 Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku.
Psaumes 45.3 Psaumes 91.5 Esaïe 27.3 Psaumes 149.5-149.9 1 Thessaloniciens 5.6-5.8 9 Mfalme Sulemani alijifanyizia machela Ya miti ya Lebanoni;
Cantique 3.7 2 Samuel 23.5 Apocalypse 14.6 10 Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu.
Apocalypse 1.5 Cantique 1.5 Romains 5.8 Ephésiens 3.18-3.19 Apocalypse 3.12 11 Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alivyovikwa na mamaye, Siku ya maposo yake, Siku ya furaha ya moyo wake.
Esaïe 62.5 Osée 2.19-2.20 Jérémie 2.2 Esaïe 4.4 Esaïe 9.6