1 Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.
Ruth 3.12 Deutéronome 25.7 Job 29.7 Deutéronome 16.18 Zacharie 2.6
2 Kisha akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, Ninyi nanyi, ketini hapa. Wakaketi.
Proverbes 31.23 1 Rois 21.8 Actes 6.12 Lamentations 5.14 Deutéronome 31.28
3 Kisha akamwambia yule jamaa, Huyu Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi aliyokuwa nayo ndugu yetu, Elimeleki;
Proverbes 13.10 Psaumes 112.5
4 nami ilikuwa nia yangu nikujulishe wewe, na kukuambia, Uinunue mbele ya hawa waliopo na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya, uikomboe; lakini kama hutaikomboa, uniambie ili nijue mimi; kwa kuwa hakuna mtu wa kuikomboa ila wewe, na baada yako ni mimi. Naye akasema, Nitaikomboa mimi.
Lévitique 25.25-25.29 Jérémie 32.7-32.12 Philippiens 4.8 Jérémie 32.25 Romains 12.17
5 Ndipo Boazi aliposema, Siku ile utakapolinunua shamba mkononi mwa Naomi, unamnunua Ruthuu pia, huyu Mmoabi, mkewe marehemu, ili makusudi umwinulie marehemu jina katika urithi wake.
Deutéronome 25.5-25.6 Genèse 38.8 Matthieu 22.24 Luc 20.28 Ruth 3.12-3.13
6 Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa.
Ruth 3.13 Lévitique 25.25
7 Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadiliana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli.
Deutéronome 25.7-25.10
8 Basi yule jamaa akamwambia Boazi, Wewe ujinunulie mwenyewe. Akavua kiatu chake.
9 Naye Boazi akawaambia wale wazee na watu wote, Leo hivi ninyi ni mashahidi ya kwamba mimi nimenunua yote yaliyokuwa ya Elimeleki, na yote yaliyokuwa ya Kilioni na Maloni, mkononi mwa Naomi.
Jérémie 32.10-32.12 Genèse 23.16-23.18
10 Tena, huyu Ruthuu Mmoabi, mkewe Maloni, nimemnunua awe mke wangu, makusudi nipate kumwinulia marehemu jina katika urithi wake, jina lake marehemu lisikatike miongoni mwa ndugu zake, wala langoni pa mji wake; leo hivi ninyi ni mashahidi.
Deutéronome 25.6 Ephésiens 5.25 Malachie 2.14 Esaïe 8.2-8.3 Osée 12.12
11 Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. Bwana na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Genèse 29.32-30.24 Michée 5.2 Psaumes 127.3-127.5 Deutéronome 25.9 Genèse 35.16-35.20
12 Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye kwamba Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa Bwana katika mwanamke huyu.
Genèse 38.29 1 Chroniques 2.4 Genèse 46.12 Matthieu 1.3 1 Samuel 2.20
13 Basi Boazi akamtwaa Ruthuu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na Bwana akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.
Genèse 29.31 Genèse 33.5 Psaumes 127.3 Ruth 3.11 1 Samuel 1.27
14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
Luc 1.58 Psaumes 34.1-34.3 Ruth 4.21-4.22 2 Thessaloniciens 1.3 Psaumes 103.1-103.2
15 Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.
1 Samuel 1.8 Genèse 45.11 Esaïe 46.4 Ruth 1.16-1.18 Proverbes 18.24
16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake.
17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.
Luc 1.58-1.63
18 Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni;
1 Chroniques 2.4-2.8 Matthieu 1.3-1.6 Luc 3.33 1 Chroniques 4.1
19 na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu;
Luc 3.33 1 Chroniques 2.9-2.10 Matthieu 1.4
20 na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni;
Nombres 1.7 Luc 3.32 Matthieu 1.4
21 na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi;
Matthieu 1.5 Luc 3.32 1 Chroniques 2.11-2.12
22 na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa Daudi.
1 Chroniques 2.15 Luc 3.31 1 Samuel 16.1 Matthieu 1.6 Esaïe 11.1