Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
2 Samuel 18.3 Bible en Swahili de l’est
1 Kisha Daudi akawahesabu watu waliokuwa pamoja naye, akaweka maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia juu yao.Exode 17.9 Josué 8.10 1 Samuel 8.12 2 Daudi akawapeleka hao watu vitani, theluthi moja chini ya mkono wa Yoabu, na theluthi ya pili chini ya mkono wa Abishai, mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi ya tatu chini ya mkono wa Itai, Mgiti. Mfalme akawaambia watu, Bila shaka mimi mwenyewe nami nitatoka pamoja nanyi.Juges 7.16 2 Samuel 15.19-15.22 2 Samuel 10.7-10.10 Psaumes 118.6-118.8 Psaumes 27.1-27.3 3 Lakini watu wakasema, Wewe usitoke nje; kwa maana tukikimbia, hawatatuona sisi kuwa kitu; au tukifa nusu yetu, hawatatuona kuwa kitu; lakini wewe u wa thamani kuliko watu elfu kumi katika sisi; kwa hivyo sasa ni afadhali ukae tayari kutusaidia toka mjini.2 Samuel 21.17 Exode 17.10-17.12 Zacharie 13.7 Lamentations 4.20 2 Samuel 10.11 4 Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa elfu zao na mia zao.2 Samuel 18.24 Esaïe 28.6 2 Samuel 18.1 1 Samuel 29.2 5 Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari za Absalomu.2 Samuel 17.1-17.4 2 Samuel 17.14 Deutéronome 21.18-21.21 Psaumes 103.13 2 Samuel 16.11 6 Hivyo watu wakatoka waende nyikani ili kupigana na Israeli; na vita vikatokea ndani ya msitu wa Efraimu.Josué 17.18 Josué 17.15 Juges 12.4-12.6 7 Watu wa Israeli wakapigwa huko mbele ya watumishi wa Daudi, kukawa na maangamizo makuu huko siku ile, ya watu ishirini elfu.2 Chroniques 13.16-13.17 Proverbes 11.21 2 Samuel 2.31 2 Samuel 19.41-19.43 2 Samuel 2.26 8 Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.Exode 15.10 Josué 10.11 1 Rois 20.30 Psaumes 43.1 Juges 5.20-5.21 9 Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.2 Samuel 14.26 Marc 7.10 Job 31.3 Jérémie 48.44 Job 18.8-18.10 10 Basi mtu mmoja akaona hayo, akaenda akamwambia Yoabu, akasema, Tazama, mimi nalimwona Absalomu ametundikwa katika mwaloni. 11 Naye Yoabu akamwambia mtu yule aliyempasha habari, Je! Wewe umeona haya; Mbona, basi, hukumpiga hata nchi papo hapo? Nami ningalikupa fedha kumi na mshipi. 12 Yule mtu akamwambia Yoabu, Kama ningalipata fedha elfu mkononi mwangu, hata hivyo singalinyosha mkono wangu juu ya mwana wa mfalme; kwa maana mfalme masikioni mwetu alikuagiza wewe, na Abishai na Itai, akisema, Angalieni sana mtu awaye yote asimguse yule kijana, Absalomu.2 Samuel 18.5 13 Na tena, kama ningaliitendea roho yake kwa hila; (wala hapana neno lo lote liwezalo kufichwa mbele ya mfalme); ndipo wewe mwenyewe ungalijitenga.2 Samuel 14.19-14.20 2 Samuel 1.15-1.16 2 Samuel 4.10-4.12 Hébreux 4.13 14 Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.Matthieu 12.40 2 Samuel 18.5 Juges 4.21 Psaumes 45.5 Juges 5.26 15 Kisha vijana kumi, waliomchukulia Yoabu silaha zake wakamzunguka, wakampiga Absalomu, na kumwua. 16 Kisha Yoabu akapiga tarumbeta, wakarudi watu toka kuwafuatia Israeli; kwani Yoabu akawazuia watu.2 Samuel 20.22 2 Samuel 2.28 1 Corinthiens 14.8 Nombres 10.2-10.10 17 Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake chungu kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.Josué 8.29 Josué 7.26 2 Samuel 19.8 2 Samuel 20.1 2 Samuel 20.22 18 Huyo Absalomu alipokuwa yu hai alikuwa ameitwaa na kujiinulia ile nguzo iliyoko bondeni mwa mfalme; kwa maana alisema, Mimi sina mtoto wa kulikumbusha jina langu; akaiita hiyo nguzo kwa jina lake mwenyewe nayo inaitwa ziara la Absalomu hata hivi leo.1 Samuel 15.12 Genèse 14.17 2 Samuel 14.27 Daniel 4.30 Jérémie 22.30 19 Basi Ahimaasi, mwana wa Sadoki, akasema, Niende mbio sasa, nikampelekee mfalme habari, jinsi Bwana alivyomlipiza kisasi juu ya adui zake.2 Samuel 15.36 2 Samuel 18.31 Psaumes 9.16 Psaumes 9.4 Psaumes 10.18 20 Yoabu akamwambia, Wewe hutakuwa mchukua habari leo, siku nyingine utachukua habari; lakini leo hutachukua habari, kwa sababu mwana wa mfalme amekufa.2 Samuel 18.29 2 Samuel 18.5 2 Samuel 17.16-17.21 2 Samuel 18.33 2 Samuel 18.27 21 Ndipo Yoabu akamwambia Mkushi mmoja, Nenda ukamwambie mfalme hayo uliyoyaona. Na huyo Mkushi akajiinamisha mbele ya Yoabu, akaenda zake mbio. 22 Ndipo Ahimaasi, mwana wa Sadoki, akamwambia Yoabu mara ya pili, Haidhuru, tafadhali nipe ruhusa, nipige mbio na mimi nyuma ya huyo Mkushi. Naye Yoabu akasema, Mbona wewe unataka kupiga mbio, mwanangu, kwa maana hutapata kitu kwa habari hizo unazopeleka?Ephésiens 5.4 Romains 1.28 23 Akasema, Haidhuru, nitapiga mbio. Akamwambia, Haya, piga mbio. Ndipo Ahimaasi akapiga mbio, akishika njia ya uwandani, akampita yule Mkushi.Jean 20.4 24 Basi Daudi alikuwa ameketi kati ya malango mawili; mlinzi akapanda juu hata dari ya lile lango hata ukutani, akainua macho yake, akaangalia, na tazama, mtu anakuja mbio peke yake.2 Samuel 19.8 2 Samuel 18.4 2 Samuel 13.34 Esaïe 21.6-21.9 Ezéchiel 33.2-33.7 25 Mlinzi akalia, akamwambia mfalme. Naye mfalme akasema, Kama yu peke yake, ana habari kinywani mwake. Akaja mbio, akakaribia. 26 Kisha huyo mlinzi akaona mtu mwingine anapiga mbio; mlinzi akamwita bawabu, akasema, Angalia, mtu mwingine anakuja mbio peke yake. Mfalme akasema, Huyu naye analeta habari. 27 Na huyo mlinzi akasema, Nionavyo mimi, kupiga mbio kwake yule wa kwanza ni kama kupiga mbio kwake Ahimaasi, mwana wa Sadoki. Naye mfalme akasema, Yeye ni mtu mwema, anakuja na habari njema.2 Rois 9.20 1 Rois 1.42 Romains 10.15 Proverbes 25.13 Proverbes 25.25 28 Ahimaasi akainua sauti yake, akamwambia mfalme, Amani. Akainama mbele ya mfalme kifudifudi, akasema, Ahimidiwe Bwana, Mungu wako, aliyewatoa watu hao walioiinua mikono yao juu ya bwana wangu, mfalme.Genèse 14.20 2 Samuel 14.4 2 Chroniques 20.26 Psaumes 115.1 Genèse 24.27 29 Mfalme akauliza, Je! Yule kijana, Absalomu, yu salama? Ahimaasi akajibu, Yoabu aliponituma mimi mtumishi wa mfalme, mimi mtumishi wako, naliona kishindo kikubwa, lakini sikujua sababu yake.2 Samuel 18.22 2 Samuel 20.9 2 Samuel 18.19-18.20 30 Naye mfalme akasema, Geuka, usimame hapa. Akageuka, akasimama. 31 Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana Bwana amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe.2 Samuel 18.19 Psaumes 94.1-94.4 Luc 18.7-18.8 2 Samuel 18.28 Deutéronome 32.35-32.36 32 Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana.Juges 5.31 1 Samuel 25.26 Psaumes 68.1-68.2 2 Samuel 18.29 Daniel 4.19 33 Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!2 Samuel 19.4 Proverbes 17.25 2 Samuel 12.10-12.23 Romains 9.3 Proverbes 10.1