Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 62.7
Bible en Swahili de l’est


1 Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. 2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. 3 Hata lini mtamshambulia mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja? Kama ukuta unaoinama, Kama kitalu kilicho tayari kuanguka, 4 Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani. 5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya. Tumaini langu hutoka kwake. 6 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. 7 Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu. 8 Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. 9 Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili. 10 Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang’anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni. 11 Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu, 12 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake.

Cette Bible est dans le domaine public.