Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 76
Bible en Swahili de l’est


1 Katika Yuda Mungu amejulikana, Katika Israeli jina lake ni kuu. Psaumes 4.1 Psaumes 148.13-148.14 Actes 17.23 Psaumes 98.2-98.3 Daniel 3.29
2 Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni. Genèse 14.18 Psaumes 132.13-132.14 Lamentations 2.6 Psaumes 27.5 Psaumes 9.11
3 Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta, Ngao, na upanga, na zana za vita. Psaumes 46.9 Ezéchiel 39.9-39.10 Ezéchiel 39.3-39.4 2 Chroniques 14.12-14.13 Esaïe 37.35-37.36
4 Wewe U mwenye fahari na adhama, Toka milima ya mateka. Ezéchiel 19.1-19.4 Daniel 7.17-7.28 Daniel 7.4-7.8 Jérémie 4.7 Ezéchiel 38.12-38.13
5 Wametekwa wenye moyo thabiti; Wamelala usingizi; Wala hawakuiona mikono yao Watu wote walio hodari. Esaïe 46.12 Nahum 3.18 Psaumes 13.3 Jérémie 51.39 Daniel 4.37
6 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito. Exode 15.1 Exode 15.21 Psaumes 80.16 Esaïe 37.36 Exode 15.4-15.6
7 Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe; Naye ni nani awezaye kusimama ufanyapo hasira? Nahum 1.6 Psaumes 89.7 Jérémie 10.7-10.10 1 Chroniques 16.25 Psaumes 90.11
8 Toka mbinguni ulitangaza hukumu; Nchi iliogopa, ikakaa kimya. 2 Chroniques 20.29-20.30 Habakuk 2.20 1 Chroniques 16.30 Juges 5.20 Zacharie 2.13
9 Mungu aliposimama ili kuhukumu Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia. Psaumes 25.9 1 Pierre 3.4 Psaumes 149.4 Psaumes 82.2-82.5 Jérémie 5.28
10 Maana hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi. Genèse 37.18-37.20 Exode 9.16-9.17 Actes 4.26-4.28 Matthieu 2.13-2.16 Matthieu 24.22
11 Wekeni nadhiri, mkaziondoe Kwa Bwana, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa. Psaumes 68.29 Psaumes 50.14 Ecclésiaste 5.4-5.6 Genèse 31.42 Psaumes 89.7
12 Yeye huzikata roho za wakuu; Na kuwatisha wafalme wa dunia. Psaumes 68.12 Sophonie 3.6 2 Chroniques 32.21 Psaumes 2.10 Esaïe 13.6-13.8

Cette Bible est dans le domaine public.