Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 86.8
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitajiPsaumes 31.2 Psaumes 40.17 Psaumes 142.1 Jacques 1.9-1.10 Psaumes 102.17
2 Unihifadhi nafsi yangu, Maana mimi ni mcha Mungu. Wewe uliye Mungu wangu, Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.Psaumes 4.3 Ephésiens 1.12-1.13 Psaumes 37.28 1 Pierre 5.3-5.5 1 Samuel 2.9
3 Wewe, Bwana, unifadhili, Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.Psaumes 57.1 Psaumes 88.9 Psaumes 25.5 Psaumes 56.1 Psaumes 4.1
4 Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.Psaumes 25.1 Psaumes 143.8 Esaïe 61.3 Esaïe 65.18 Psaumes 62.8
5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.Joël 2.13 Psaumes 103.8 Exode 34.6 Néhémie 9.17 Psaumes 130.7
6 Ee Bwana, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu.Psaumes 5.1-5.2 Psaumes 130.2 Psaumes 55.1 Psaumes 17.1
7 Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia.Psaumes 50.15 Jonas 2.2 Psaumes 17.6 Psaumes 34.4-34.6 Esaïe 26.16
8 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, Wala matendo mfano wa matendo yako.Exode 15.11 Psaumes 89.6 Deutéronome 3.24 Deutéronome 4.34 Esaïe 40.18
9 Mataifa yote uliowafanya watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako;Apocalypse 15.4 Psaumes 66.4 Esaïe 66.23 Psaumes 102.15 Ephésiens 1.12
10 Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe Mungu peke yako.Psaumes 72.18 Marc 12.29 Esaïe 37.16 1 Corinthiens 8.4 Deutéronome 32.39
11 Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;Jérémie 32.38-32.39 Psaumes 26.3 1 Corinthiens 6.17 1 Corinthiens 10.21 Psaumes 5.8
12 Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.Deutéronome 6.5 Romains 15.6 1 Corinthiens 10.31 Psaumes 145.1-145.5 Apocalypse 19.5-19.6
13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.Psaumes 103.8-103.12 Luc 1.58 Psaumes 30.3 Job 33.18 1 Thessaloniciens 1.10
14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao.Psaumes 54.3 Psaumes 36.11 Psaumes 14.4 Matthieu 26.3-26.4 Ezéchiel 9.9
15 Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.Psaumes 111.4 Psaumes 86.5 Psaumes 103.8 Néhémie 9.17 Ephésiens 1.7
16 Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako.Psaumes 25.16 Psaumes 116.16 Zacharie 10.12 Psaumes 69.16 Psaumes 138.3
17 Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, Bwana, Umenisaidia na kunifariji.Psaumes 41.10-41.11 Psaumes 40.1 Psaumes 71.20-71.21 Juges 6.17 1 Corinthiens 5.5

Cette Bible est dans le domaine public.