Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 17
Bible en Swahili de l’est


1 Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. Exode 16.1 Exode 19.2 Nombres 33.12-33.14 Exode 17.8
2 Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana? Deutéronome 6.16 Psaumes 78.41 Psaumes 78.18 Matthieu 4.7 1 Corinthiens 10.9
3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Exode 16.2-16.3 Exode 15.24
4 Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. Nombres 14.10 1 Samuel 30.6 Jean 10.31 Jean 8.59 Actes 14.19
5 Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende. Actes 20.23-20.24 Exode 7.19-7.20 Nombres 20.8-20.11 Ezéchiel 2.6
6 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. 1 Corinthiens 10.4 Psaumes 105.41 Psaumes 114.8 Nombres 20.9-20.11 Jean 7.37-7.38
7 Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je! Bwana yu kati yetu au sivyo? Psaumes 81.7 Nombres 20.13 Psaumes 95.8 Deutéronome 9.22 Exode 17.2
8 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. 1 Samuel 15.2 Genèse 36.12 Nombres 24.20 Deutéronome 25.17-25.19 1 Samuel 30.1
9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Exode 4.20 Exode 24.13 Exode 4.2 Deutéronome 32.44 Hébreux 4.8
10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Exode 24.14 Exode 31.2 Matthieu 28.20 Jean 2.5 Exode 17.12
11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Jacques 5.16 1 Timothée 2.8 Psaumes 56.9 Luc 18.1
12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Esaïe 35.3 1 Thessaloniciens 5.25 Philippiens 1.19 Colossiens 4.2 2 Corinthiens 1.11
13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. Josué 10.37 Josué 10.32 Josué 10.42 Josué 11.12 Josué 10.28
14 Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. 1 Samuel 30.17 Exode 34.27 Nombres 24.20 2 Samuel 8.12 1 Samuel 30.1
15 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi; Genèse 22.14 Psaumes 60.4 Juges 6.24 Genèse 33.20
16 akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi. Esaïe 66.1 Psaumes 21.8-21.11 Actes 7.49

Cette Bible est dans le domaine public.