Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 11
Bible en Swahili de l’est


1 Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri. Matthieu 2.15 Exode 4.22 Osée 2.15 Jérémie 2.2 Deutéronome 7.7
2 Kadiri walivyowaita ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu Mabaali, na kuzifukizia uvumba sanamu za kuchonga. Osée 2.13 Jérémie 18.15 Esaïe 65.7 Osée 11.7 Osée 13.1-13.2
3 Lakini nalimfundisha Efraimu kwenda kwa miguu; naliwachukua mikononi mwangu; hawakujua ya kuwa naliwaponya. Deutéronome 1.31 Jérémie 30.17 Exode 15.26 Osée 14.4 Osée 2.8
4 Naliwavuta kwa kamba za kibinadamu, kwa mafungo ya upendo; nami nalikuwa kwao kama hao waondoao kongwa tayani mwao, nikaandika chakula mbele yao. Lévitique 26.13 Jean 12.32 Exode 16.32 Jérémie 31.2-31.3 2 Samuel 7.14
5 Hatarudi tena nchi ya Misri; bali huyo Mwashuri atakuwa mfalme wake; kwa sababu walikataa kurejea. Osée 7.16 Osée 8.13 2 Rois 17.13-17.14 Osée 9.3 Osée 10.6
6 Na upanga utaiangukia miji yake, utayaharibu makomeo yake na kuyala, kwa sababu ya mashauri yao wenyewe. Osée 13.16 Osée 10.14 Osée 10.6 Ezéchiel 15.2-15.7 Esaïe 27.10
7 Na watu wangu wamejipinda kuniacha; ingawa wawaita kwenda kwake Aliye juu, hapana hata mmoja atakayemtukuza. Jérémie 8.5 Psaumes 78.57-78.58 Amos 5.4-5.6 Osée 14.4 Psaumes 81.11
8 Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuponya, Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu ? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja. Deutéronome 29.23 Genèse 14.8 Osée 6.4 Matthieu 23.37 Jérémie 31.20
9 Sitatumia ukali wa hasira yangu, sitarudi kumwangamiza Efraimu; kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji. Nombres 23.19 Esaïe 12.6 Jérémie 30.11 Exode 32.10-32.14 Malachie 3.6
10 Watakwenda kumfuata Bwana, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka. Esaïe 31.4 Joël 3.16 Amos 1.2 Jérémie 25.30 Zacharie 8.7
11 Watakuja wakitetemeka kama shomoro, toka Misri, na kama hua, toka nchi ya Ashuru; nami nitawakalisha katika nyumba zao, asema Bwana. Esaïe 11.11 Esaïe 60.8 Zacharie 10.10 Osée 7.11 Amos 9.14-9.15
12 Efraimu amenizinga kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu; na Yuda hata sasa anasita-sita kwa Mungu, na kwake aliye Mtakatifu, naye ni mwaminifu. Apocalypse 1.6 Esaïe 29.13 Michée 6.12 Osée 12.7 Esaïe 59.3-59.4

Cette Bible est dans le domaine public.