Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Corinthiens 6.19
Bible en Swahili de l’est


1 Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?Actes 18.14-18.15 Actes 19.38 1 Corinthiens 16.1 Matthieu 18.15-18.17 1 Corinthiens 14.33
2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?Matthieu 19.28 Apocalypse 20.4 Luc 22.30 Apocalypse 2.26-2.27 Daniel 7.22
3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?Luc 8.14 Matthieu 25.41 Jude 1.6 Luc 21.34 1 Corinthiens 6.4
4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?1 Corinthiens 5.12 Actes 6.2-6.4
5 Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?1 Corinthiens 4.14 1 Corinthiens 15.34 Jacques 3.13-3.18 Proverbes 14.8 1 Corinthiens 3.18
6 Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini.1 Jean 3.11-3.15 Actes 7.26 Genèse 45.24 1 Corinthiens 6.7 Psaumes 133.1-133.3
7 Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?Proverbes 20.22 1 Pierre 3.9 1 Pierre 2.19-2.23 Jacques 4.1-4.3 Romains 12.17-12.19
8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.1 Thessaloniciens 4.6 Marc 10.19 Colossiens 3.25 Malachie 3.5 Michée 2.2
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,Galates 5.19-5.21 1 Timothée 1.9-1.10 Lévitique 20.13 Ephésiens 5.4-5.5 Lévitique 18.22
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.1 Corinthiens 5.11 Galates 5.21 Ezéchiel 22.27 Matthieu 23.33 Ezéchiel 22.29
11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.1 Corinthiens 1.2 Actes 22.16 Ephésiens 5.26 Hébreux 10.22 Romains 8.30
12 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.1 Corinthiens 10.23-10.33 1 Corinthiens 9.27 Romains 14.14-14.23 1 Corinthiens 8.7-8.13 Hébreux 12.15-12.16
13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.1 Corinthiens 6.15 1 Corinthiens 6.19 Matthieu 15.17 Ephésiens 5.23 1 Corinthiens 3.16
14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.Actes 2.24 Ephésiens 1.19-1.20 Jean 6.39-6.40 Jean 5.28-5.29 Romains 8.11
15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!Romains 12.5 Ephésiens 5.30 1 Corinthiens 12.27 Luc 20.16 Ephésiens 4.15-4.16
16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.Genèse 2.24 Ephésiens 5.31 Marc 10.8 Matthieu 19.5-19.6 Juges 16.1
17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.Jean 17.21-17.23 1 Corinthiens 12.13 Jean 3.6 Ephésiens 4.3-4.4 Galates 2.20
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.Hébreux 13.4 Colossiens 3.5 1 Thessaloniciens 4.3 Romains 6.12-6.13 1 Pierre 2.11
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;1 Corinthiens 3.16 2 Corinthiens 6.16 1 Pierre 2.5 Ephésiens 2.21-2.22 Jean 2.21
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.1 Corinthiens 7.23 Romains 12.1 1 Pierre 1.18 1 Pierre 2.9 Actes 20.28

Cette Bible est dans le domaine public.