Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Apocalypse 18.4
Bible en Swahili de l’est


1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.Ezéchiel 43.2 Apocalypse 17.1 Esaïe 60.1-60.3 Luc 17.24 Apocalypse 21.23
2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;Apocalypse 14.8 Jérémie 51.37 Jérémie 50.39-50.40 Esaïe 14.23 Jérémie 51.8
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.Apocalypse 14.8 Apocalypse 17.2 Apocalypse 18.9 Ezéchiel 27.9-27.25 Jérémie 51.7
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.2 Corinthiens 6.17 Jérémie 51.6 Jérémie 51.45 Esaïe 52.11 Jérémie 50.8
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.Apocalypse 16.19 Jérémie 51.9 Esdras 9.6 Genèse 18.20-18.21 Jonas 1.2
6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.Psaumes 137.8 Jérémie 50.15 Jérémie 50.29 Apocalypse 16.19 Apocalypse 17.4
7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.Sophonie 2.15 Lamentations 1.1 Psaumes 45.9 Esaïe 22.12-22.14 Esaïe 47.7-47.9
8 Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.Jérémie 50.34 Jérémie 50.31 Apocalypse 17.16 Apocalypse 18.9-18.10 Apocalypse 11.17
9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;Apocalypse 19.3 Apocalypse 18.3 Apocalypse 17.2 Apocalypse 18.18 Ezéchiel 26.16-26.17
10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.Apocalypse 18.19 Apocalypse 18.8 Apocalypse 18.15-18.17 Apocalypse 14.8 Joël 1.15
11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;Apocalypse 18.3 Apocalypse 18.15 Ezéchiel 27.27-27.36 Apocalypse 18.23 Esaïe 23.1-23.15
12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;Apocalypse 17.4 Ezéchiel 27.5-27.25 Proverbes 8.10-8.11 2 Chroniques 2.8 1 Rois 10.11-10.12
13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.Ezéchiel 27.13 Néhémie 5.8 1 Timothée 1.10 Amos 2.6 Esaïe 50.1
14 Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.Luc 16.25 Jacques 4.2 Psaumes 106.14 Psaumes 78.18 1 Jean 2.16-2.17
15 Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza,Apocalypse 18.3 Ezéchiel 27.31 Actes 19.24-19.27 Juges 18.23-18.24 Osée 12.7-12.8
16 wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu;Apocalypse 17.4 Apocalypse 18.10-18.11 Apocalypse 18.19 Luc 16.19-16.31
17 kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali;Jonas 1.6 Apocalypse 17.16 Esaïe 23.14 Ezéchiel 27.27-27.36 Lamentations 4.6
18 wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!Apocalypse 13.4 Apocalypse 18.9-18.10 Ezéchiel 27.30-27.32 Jérémie 51.37 Esaïe 23.8-23.9
19 Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.Apocalypse 18.10 Josué 7.6 Job 2.12 Ezéchiel 27.30 Néhémie 9.1
20 Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii; kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.Apocalypse 12.12 Apocalypse 6.10 Luc 11.49-11.50 Luc 18.7-18.8 Jérémie 51.47-51.48
21 Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.Apocalypse 5.2 Jérémie 51.63-51.64 Ezéchiel 26.21 Job 20.8 Psaumes 37.36
22 Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;Ezéchiel 26.13 Jérémie 25.10 Jérémie 7.34 Jérémie 33.11 Esaïe 24.8-24.9
23 wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.Apocalypse 18.3 Esaïe 23.8 Nahum 3.4 Jérémie 7.34 Jérémie 16.9
24 Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.Apocalypse 17.6 Apocalypse 16.6 Jérémie 51.49 Ezéchiel 22.12 Matthieu 23.35

Cette Bible est dans le domaine public.