Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
2 Samuel 21 Bible en Swahili de l’est
Vengeance des Gabaonites
1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni. Genèse 12.10 Nombres 27.21 Genèse 26.1 Psaumes 91.15 Job 10.2 2 Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;) 2 Rois 10.16 Galates 4.17 1 Samuel 14.44 Deutéronome 7.16 Genèse 15.16 3 basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa Bwana? 2 Samuel 20.19 1 Samuel 26.19 Hébreux 10.4-10.12 Michée 6.6-6.7 1 Samuel 2.25 4 Na hao Wagibeoni wakamwambia, Si jambo la fedha wala dhahabu lililo kati ya sisi na Sauli, au nyumba yake; wala si juu yetu kumwua mtu ye yote katika Israeli. Akasema Mtakayoyanena, ndiyo nitakayowatendea ninyi. Psaumes 49.6-49.8 1 Pierre 1.18-1.19 5 Wakamwambia mfalme, Yule mtu aliyetupoteza, na kutufanyia shauri la kutuharibu, tusikae katika mipaka yo yote ya Israeli, 2 Samuel 21.1 Daniel 9.26 Matthieu 7.2 Esther 9.24-9.25 6 basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za Bwana katika Gibeoni, katika mlima wa Bwana. Mfalme akasema, Nitawatoa. 1 Samuel 10.24 1 Samuel 10.26 1 Samuel 11.4 Nombres 25.4-25.5 2 Samuel 17.23 7 Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Bwana kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli. 1 Samuel 20.15 1 Samuel 18.3 1 Samuel 20.8 2 Samuel 4.4 1 Samuel 23.18 8 Ila mfalme akawatwaa hao wana wawili wa Rispa, binti Aya, aliomzalia Sauli, Armoni na Mefiboshethi; na wana watano wa Merabu binti Sauli, aliomzalia Adrieli, mwana wa Barzilai, Mmeholathi; 2 Samuel 3.7 1 Samuel 18.19 9 akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za Bwana, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri. Ruth 1.22 2 Samuel 21.6 Exode 20.5 Nombres 35.31-35.34 2 Samuel 6.21 10 Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku. Deutéronome 21.23 2 Samuel 3.7 Genèse 40.19 1 Rois 21.27 Ezéchiel 39.4 11 Kisha akaambiwa Daudi hayo aliyoyafanya huyo Rispa binti Aya, suria wa Sauli. 2 Samuel 2.4 Ruth 2.11-2.12 12 Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa; 1 Samuel 31.10-31.13 Josué 17.11 1 Samuel 31.1 1 Chroniques 10.1 1 Samuel 28.4 13 naye akaileta toka huko hiyo mifupa ya Sauli, na mifupa ya Yonathani mwanawe; nao wakaizoa mifupa yao waliotundikwa. 14 Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi. 2 Samuel 24.25 Josué 18.28 Josué 7.26 Amos 7.1-7.6 2 Samuel 3.32