Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
2 Samuel 21.18 Bible en Swahili de l’est
Vengeance des Gabaonites
1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni. Nombres 27.21 Genèse 12.10 Genèse 26.1 2 Rois 8.1 Lévitique 26.26 2 Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;) Luc 9.54-9.55 Jean 16.2 2 Rois 10.16 Galates 4.17 1 Samuel 14.44 3 basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa Bwana? 2 Samuel 20.19 1 Samuel 26.19 Hébreux 9.22 Hébreux 10.4-10.12 Michée 6.6-6.7 4 Na hao Wagibeoni wakamwambia, Si jambo la fedha wala dhahabu lililo kati ya sisi na Sauli, au nyumba yake; wala si juu yetu kumwua mtu ye yote katika Israeli. Akasema Mtakayoyanena, ndiyo nitakayowatendea ninyi. Psaumes 49.6-49.8 1 Pierre 1.18-1.19 5 Wakamwambia mfalme, Yule mtu aliyetupoteza, na kutufanyia shauri la kutuharibu, tusikae katika mipaka yo yote ya Israeli, 2 Samuel 21.1 Esther 9.24-9.25 Daniel 9.26 Matthieu 7.2 6 basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za Bwana katika Gibeoni, katika mlima wa Bwana. Mfalme akasema, Nitawatoa. 1 Samuel 10.24 1 Samuel 11.4 Nombres 25.4-25.5 1 Samuel 10.26 Matthieu 27.5 7 Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Bwana kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli. 1 Samuel 20.15 1 Samuel 18.3 1 Samuel 20.8 2 Samuel 4.4 1 Samuel 23.18 8 Ila mfalme akawatwaa hao wana wawili wa Rispa, binti Aya, aliomzalia Sauli, Armoni na Mefiboshethi; na wana watano wa Merabu binti Sauli, aliomzalia Adrieli, mwana wa Barzilai, Mmeholathi; 2 Samuel 3.7 1 Samuel 18.19 9 akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za Bwana, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri. Ruth 1.22 2 Rois 24.3-24.4 1 Samuel 15.33 2 Samuel 21.6 Exode 20.5 10 Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku. 2 Samuel 3.7 Deutéronome 21.23 Zacharie 10.1 Osée 6.3 Deutéronome 11.14 11 Kisha akaambiwa Daudi hayo aliyoyafanya huyo Rispa binti Aya, suria wa Sauli. 2 Samuel 2.4 Ruth 2.11-2.12 12 Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa; Josué 17.11 1 Samuel 31.10-31.13 2 Samuel 1.21 1 Samuel 31.1 1 Chroniques 10.1 13 naye akaileta toka huko hiyo mifupa ya Sauli, na mifupa ya Yonathani mwanawe; nao wakaizoa mifupa yao waliotundikwa. 14 Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi. Josué 18.28 2 Samuel 24.25 Josué 7.26 Jérémie 14.1-14.7 1 Samuel 10.2