Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Samuel 9
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani? 1 Samuel 20.42 1 Samuel 20.14-20.17 Jean 19.26-19.27 Matthieu 25.40 1 Rois 2.7
2 Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye. 2 Samuel 16.1-16.4 2 Samuel 19.17 Genèse 39.6 Genèse 24.2 Genèse 15.2-15.3
3 Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu. 2 Samuel 4.4 1 Samuel 20.14-20.17 Deutéronome 10.15 Luc 6.36 Tite 3.3-3.4
4 Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 2 Samuel 17.27-17.29
5 Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 6 Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako! 1 Chroniques 8.34 1 Chroniques 9.40 2 Samuel 16.4 2 Samuel 19.24-19.30 1 Samuel 25.23
7 Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima. 2 Samuel 19.28 2 Samuel 9.1 1 Rois 2.7 2 Samuel 9.3 2 Rois 25.29
8 Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi? 2 Samuel 16.9 1 Samuel 24.14-24.15 Matthieu 15.26-15.27 1 Samuel 26.20 2 Samuel 3.8
9 Ndipo mfalme akamwita Siba, mtumwa wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake nimempa mwana wa bwana wako. 2 Samuel 19.29 2 Samuel 16.4 1 Samuel 9.1 Esaïe 32.8
10 Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumwa wako; nawe utamletea mwana wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mwana wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu sikuzote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumwa ishirini. 2 Samuel 9.7 2 Samuel 19.28 Luc 14.15 2 Samuel 9.11-9.13 2 Rois 25.29
11 Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumwa wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kwa habari za Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme. 2 Samuel 19.26 2 Samuel 16.1-16.4 2 Samuel 19.17
12 Huyo Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumwa wa Mefiboshethi. Michée 7.5-7.6 1 Chroniques 8.34-8.40 1 Chroniques 9.40-9.44 1 Chroniques 8.8
13 Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula sikuzote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili. 2 Samuel 9.7 2 Samuel 9.3 2 Samuel 9.10-9.11

Cette Bible est dans le domaine public.