8 Katika mwaka wa ishirini na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha alianza kutawala juu ya Israeli huko Tirza, akatawala miaka miwili. 9 Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamfanyia fitina; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza; Genèse 39.4 1 Rois 18.3 Genèse 24.2 Nahum 1.10 2 Rois 15.10 10 Zimri akaingia akampiga, akamwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala mahali pake. 2 Rois 9.31 11 Ikawa, alipoanza kutawala, mara alipoketi juu ya kiti chake cha enzi, akawaua nyumba yote ya Baasha; hakumwachia mwanamume ye yote, wa jamaa zake, wala wa rafiki zake. 1 Rois 15.29 1 Samuel 25.22 1 Rois 16.3 1 Samuel 25.34 1 Rois 14.10 12 Hivyo Zimri akaiharibu nyumba yote ya Baasha, sawasawa na neno la Bwana, alilolinena juu ya Baasha kwa Yehu nabii, 1 Rois 16.1 1 Rois 16.3 Proverbes 26.6 2 Chroniques 10.15 2 Rois 14.25 13 kwa sababu ya makosa yake Baasha, na makosa yote ya Ela mwanawe, waliyoyakosa, na kuwakosesha Israeli, wakimghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kwa matendo yao ya ubatili. Deutéronome 32.21 Esaïe 41.29 1 Samuel 12.21 1 Rois 15.30 Jérémie 10.3-10.5 14 Na mambo yote ya Ela yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?
29 Ahabu mwana wa Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na nane wa Asa mfalme wa Yuda; akatawala Ahabu mwana wa Omri juu ya Israeli katika Samaria miaka ishirini na miwili. 30 Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana kuliko wote waliomtangulia. 1 Rois 16.25 1 Rois 14.9 1 Rois 21.25 2 Rois 3.2 1 Rois 16.31 31 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia. 2 Rois 17.16 2 Rois 10.18 Juges 18.7 Deutéronome 7.3-7.4 1 Rois 21.25-21.26 32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria. 2 Rois 10.21 2 Rois 10.26-10.27 33 Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia. 2 Rois 13.6 1 Rois 21.25 Exode 34.13 2 Rois 21.3 1 Rois 22.8 34 Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni. Josué 6.26 Matthieu 24.35 Zacharie 1.5 Josué 23.14-23.15