8 Hata mwaka wa pili wa kufika kwao nyumbani kwa Mungu, huko Yerusalemu, mwezi wa pili, Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zao wengine, makuhani na Walawi, na watu wote, waliotoka katika uhamisho na kufika Yerusalemu, wakaanza; nao wakawaweka Walawi, hao wenye miaka ishirini na waliozidi, ili kuisimamia kazi ya nyumba ya Bwana. 1 Chroniques 23.24-23.32 1 Chroniques 23.4 Esdras 4.3 Nombres 4.3 9 Ndipo wakasimama Yeshua, na wanawe na ndugu zake, Kadmieli, na wanawe, wana wa Hodavia, pamoja, ili kuwasimamia hao wafanyao kazi katika nyumba ya Mungu; wana wa Henadadi, pamoja na wana wao, na ndugu zao, Walawi. Esdras 2.40 Néhémie 7.43 Esdras 3.8 10 Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la Bwana, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi Bwana, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli. Zacharie 4.10 1 Chroniques 16.4-16.7 1 Chroniques 25.1-25.7 2 Chroniques 29.25-29.26 Néhémie 12.24-12.26 11 Wakaimbiana, wakimhimidi Bwana, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana umekwisha kuwekwa. 1 Chroniques 16.34 Psaumes 107.1 Néhémie 12.24 2 Chroniques 7.3 Jérémie 33.11 12 Bali makuhani wengi, na Walawi, na wakuu wa mbari za mababa, waliokuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakati msingi wa nyumba hii ulipowekwa mbele ya macho yao, walilia kwa sauti kuu; na watu wengi walipiga kelele za furaha; Aggée 2.3 Matthieu 13.31-13.32 Esaïe 60.22 Zacharie 4.10 Jérémie 31.8-31.9 13 hata watu wasiweze kupambanua kelele za furaha, na kelele za vilio vya watu; maana watu walipiga kelele kwa sauti kuu, na kelele zao zikasikilikana mbali sana. Zacharie 4.7 1 Rois 1.40 1 Samuel 4.5 Luc 19.37-19.40 1 Rois 1.45