Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Esther 5.13 Bible en Swahili de l’est
Démarche d’Esther auprès du roi
1 Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba. Esther 4.16 Esther 6.4 Esther 4.11 1 Pierre 3.3-3.5 Luc 22.30 2 Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo. Esther 8.4 Esther 4.11 Proverbes 21.1 Psaumes 116.1 Actes 7.10 3 Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme. Marc 6.23 Esther 7.2 Esther 5.6 Esther 9.12 Matthieu 20.20-20.22 4 Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia. Esther 5.8 Proverbes 29.11 Genèse 32.20 1 Corinthiens 14.20 Psaumes 112.5 5 Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili ifanyike kama Esta alivyosema. Hivyo mfalme na Hamani wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta. Esther 6.14 6 Basi mfalme akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa. Esther 7.2 Esther 9.12 Esther 5.3 7 Esta akajibu, na kusema, Dua yangu ni hii, na haja yangu ni hii, 8 Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunifanyizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema. Esther 7.3 Esther 6.1-6.14 Esther 8.5 Proverbes 16.9