1 Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba.
Esther 4.16 Esther 6.4 Esther 4.11 1 Pierre 3.3-3.5 Luc 22.30
2 Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.
Esther 8.4 Esther 4.11 Proverbes 21.1 Psaumes 116.1 Actes 7.10
3 Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme.
Marc 6.23 Esther 7.2 Esther 5.6 Esther 9.12 Matthieu 20.20-20.22
4 Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia.
Esther 5.8 Proverbes 29.11 Genèse 32.20 1 Corinthiens 14.20 Psaumes 112.5
5 Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili ifanyike kama Esta alivyosema. Hivyo mfalme na Hamani wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
Esther 6.14
6 Basi mfalme akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa.
Esther 7.2 Esther 9.12 Esther 5.3
7 Esta akajibu, na kusema, Dua yangu ni hii, na haja yangu ni hii,
8 Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunifanyizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.
Esther 7.3 Esther 6.1-6.14 Esther 8.5 Proverbes 16.9
9 Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai.
Esther 3.5 Daniel 3.13 Jean 16.20 Amos 6.12-6.13 Actes 7.54
10 Walakini Hamani akajizuia, akaenda zake nyumbani kwake; akatuma kuwaita rafiki zake na Zereshi mkewe.
Esther 6.13 Ecclésiaste 7.9 Genèse 45.1 Genèse 43.30-43.31 2 Samuel 13.22-13.23
11 Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, nayo mambo yote pia ambayo mfalme amemfanikisha katika hayo, na jinsi alivyompandisha juu ya maakida na watumishi wa mfalme.
Esther 9.7-9.10 Esther 3.1 Luc 12.19-12.20 Psaumes 49.6 Psaumes 49.16-49.17
12 Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme.
Proverbes 27.1 Psaumes 37.35-37.36 Proverbes 7.22-7.23 Luc 21.34-21.35 Job 20.5-20.8
13 Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme?
Philippiens 4.11-4.12 Job 15.20 Job 18.4 Ecclésiaste 1.2 Ecclésiaste 1.14
14 Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.Esther 6.4 Esther 7.9-7.10 1 Rois 21.7 Psaumes 7.13-7.16 Psaumes 37.14