Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Job 23.4 Bible en Swahili de l’est
Intervention n° 8 de Job
1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Hata leo mashitaka yangu yana uchungu; Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu. 3 Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona, Nifike hata hapo anapokaa! 4 Ningeiweka daawa yangu mbele yake, Na kukijaza kinywa changu hoja. 5 Ningeyajua maneno atakayonijibu, Na kuelewa na hayo atakayoniambia. 6 Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza. 7 Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele. 8 Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; 9 Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone. 10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. 11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. 12 Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu, 13 Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo. 14 Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa; Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye. 15 Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake; Nitakapofikiri, namwogopa. 16 Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia, Naye Mwenyezi amenitaabisha; 17 Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza, Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.