Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 36
Bible en Swahili de l’est


1 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. Romains 3.18 Psaumes 18.1 Proverbes 20.11 Apocalypse 1.1 2 Pierre 1.1
2 Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa. Deutéronome 29.19 Psaumes 49.18 Psaumes 10.3 Romains 7.9 Osée 12.7-12.8
3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema. Psaumes 55.21 Jérémie 4.22 Psaumes 10.7 1 Samuel 19.6-19.7 Psaumes 94.8
4 Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii. Proverbes 4.16 Esaïe 65.2 Michée 2.1 Romains 12.9 Psaumes 97.10
5 Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni. Psaumes 57.10 Psaumes 103.11 Psaumes 108.4 Psaumes 52.1 Esaïe 55.7-55.9
6 Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama. Romains 11.33 Psaumes 77.19 Psaumes 71.19 Psaumes 145.9 Psaumes 92.5
7 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako. Ruth 2.12 Psaumes 91.4 Psaumes 17.8 Psaumes 139.17 Psaumes 31.19
8 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako. Psaumes 65.4 Psaumes 16.11 Esaïe 25.6 Jérémie 31.12-31.14 Esaïe 58.11
9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru. Jérémie 2.13 1 Pierre 2.9 Jean 4.14 Jean 4.10 1 Jean 1.7
10 Uwadumishie wakujuao fadhili zako, Na wanyofu wa moyo uaminifu wako. Jérémie 22.16 Psaumes 97.10-97.11 Jérémie 31.3 Psaumes 9.10 Psaumes 103.17
11 Mguu wa kiburi usinikaribie, Wala mkono wa wasio haki usinifukuze. Psaumes 10.2 Psaumes 119.51 Psaumes 62.6 Esaïe 51.23 Psaumes 119.85
12 Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama. Psaumes 1.5 Apocalypse 19.1-19.6 2 Thessaloniciens 1.8-1.9 Psaumes 140.10 Psaumes 18.38

Cette Bible est dans le domaine public.