Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 36.5
Bible en Swahili de l’est


1 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.Romains 3.18 Psaumes 18.1 Tite 1.16 Genèse 20.11 Matthieu 7.16-7.20
2 Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.Psaumes 49.18 Deutéronome 29.19 Psaumes 10.3 Jérémie 17.9 Romains 3.9
3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.Psaumes 10.7 Psaumes 55.21 Jérémie 4.22 1 Samuel 26.21 1 Samuel 15.26
4 Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.Michée 2.1 Proverbes 4.16 Esaïe 65.2 Romains 12.9 Psaumes 97.10
5 Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni.Psaumes 57.10 Psaumes 103.11 Psaumes 108.4 Hébreux 6.18-6.20 Matthieu 24.35
6 Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama.Romains 11.33 Psaumes 71.19 Psaumes 77.19 Psaumes 92.5 Psaumes 145.9
7 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.Ruth 2.12 Psaumes 91.4 Psaumes 17.8 1 Jean 3.1 Psaumes 139.17
8 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.Psaumes 65.4 Psaumes 16.11 Esaïe 25.6 Jérémie 31.12-31.14 Psaumes 63.5
9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru.Jérémie 2.13 1 Pierre 2.9 Jean 4.14 Jean 4.10 Jacques 1.17
10 Uwadumishie wakujuao fadhili zako, Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.Jérémie 22.16 Psaumes 97.10-97.11 Psaumes 94.14-94.15 Jérémie 24.7 Esaïe 51.6-51.8
11 Mguu wa kiburi usinikaribie, Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.Romains 8.35-8.39 Psaumes 125.1-125.3 Psaumes 123.3-123.4 Psaumes 12.3-12.5 Psaumes 16.8
12 Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama.Psaumes 1.5 Jérémie 51.64 Juges 5.31 Psaumes 64.7-64.9 Apocalypse 19.1-19.6

Cette Bible est dans le domaine public.