1 Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki? Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?
Psaumes 57.1 Matthieu 26.3 Psaumes 82.1-82.2 Psaumes 59.1 Deutéronome 1.15-1.16
2 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu; Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.
Psaumes 94.20 Esaïe 10.1 Michée 3.9-3.12 Ezéchiel 22.12 Jean 11.47-11.53
3 Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
Psaumes 51.5 Esaïe 48.8 Esaïe 46.3 Proverbes 22.15 Ephésiens 2.3
4 Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka; Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.
Psaumes 140.3 Ecclésiaste 10.11 Job 20.14 Romains 3.13 Jacques 3.8
5 Asiyeisikiliza sauti ya waganga, Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.
Deutéronome 18.11 Esaïe 19.3 Jérémie 8.17
6 Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao; Ee Bwana, uyavunje magego ya wana-simba.
Psaumes 3.7 Job 29.17 Nombres 23.24 Job 4.10-4.11 Ezéchiel 30.21-30.26
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi; Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.
Psaumes 112.10 Josué 7.5 Esaïe 13.7 Psaumes 64.3 Josué 2.9-2.11
8 Kama konokono ayeyukaye na kutoweka, Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,
Job 3.16 Ecclésiaste 6.3 Jacques 1.10 Psaumes 37.35-37.36 Matthieu 24.35
9 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.Proverbes 10.25 Psaumes 118.12 Ecclésiaste 7.6 Job 20.5-20.29 Jérémie 23.19
10 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi; Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.
Psaumes 68.23 Psaumes 64.10 Psaumes 107.42 Deutéronome 32.43 Psaumes 68.1-68.3
11 Na mwanadamu atasema, Hakika iko thawabu yake mwenye haki. Hakika yuko Mungu Anayehukumu katika dunia.
Esaïe 3.10 Psaumes 67.4 Psaumes 9.16 Malachie 3.14 Psaumes 18.20