Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 21
Bible en Swahili de l’est


1 Ufunuo juu ya bara ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi,inakuja kutoka bara,toka nchi itishayo. Esaïe 13.1 Jérémie 51.42 Zacharie 9.14 Esaïe 13.20-13.22 Esaïe 14.23
2 Nimeonyeshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote. Esaïe 33.1 Jérémie 49.34 Psaumes 60.3 Esaïe 24.16 Zacharie 1.15-1.16
3 Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, utungu umenishika, kama utungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona. Esaïe 13.8 Psaumes 48.6 Esaïe 26.17 Michée 4.9-4.10 Jérémie 48.41
4 Moyo wangu unapiga-piga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha. Luc 21.34-21.36 Jérémie 51.57 Esther 5.12 1 Samuel 25.36-25.38 Jérémie 51.39
5 Wanaandika meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta. Jérémie 51.57 Jérémie 51.39 1 Corinthiens 15.32 Daniel 5.1-5.5 Jérémie 51.11
6 Maana Bwana ameniambia hivi, Enenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze. 2 Rois 9.17-9.20 Ezéchiel 3.17 Ezéchiel 33.2-33.7 Jérémie 51.12-51.13 Habakuk 2.1-2.2
7 Naye akiona kundi la wapanda farasi, wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia; asikilize sana, akijitahidi kusikiliza. Esaïe 21.9 Hébreux 2.1 Esaïe 37.24
8 Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu. Habakuk 2.1-2.2 Jérémie 50.44 Jérémie 4.7 Jérémie 25.38 1 Pierre 5.8
9 Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini. Apocalypse 18.2 Jérémie 51.8 Apocalypse 14.8 Jérémie 51.44 Esaïe 13.19
10 Ewe niliyekufikicha, na nafaka ya sakafu yangu; Hayo niliyoyasikia kwa Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, nimewapasha habari zake. Jérémie 51.33 Michée 4.13 Matthieu 3.12 Esaïe 41.15-41.16 2 Rois 13.7
11 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku? Genèse 25.14 1 Chroniques 1.30 Genèse 32.3 Abdias 1.1-1.16 Jérémie 37.17
12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena. Actes 17.30-17.32 Ezéchiel 7.12 Ezéchiel 7.5-7.7 Ezéchiel 18.30-18.32 Actes 17.19-17.20
13 Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani. Jérémie 25.23-25.24 Genèse 25.3 Ezéchiel 27.15 Ezéchiel 27.20-27.21 1 Chroniques 1.32
14 Waleteeni wenye kiu maji, Enyi wenyeji wa nchi ya Tema; Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao. Job 6.19 Genèse 25.15 1 Pierre 4.9 Esaïe 16.3-16.4 Romains 12.20
15 Kwa maana wanakimbia mbele ya panga, Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa, Na mbele ya ukali wa vita. Esaïe 13.14 Job 6.19-6.20
16 Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari. Esaïe 60.7 Esaïe 16.14 Psaumes 120.5 Cantique 1.5 Ezéchiel 27.21
17 Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana Bwana, Mungu wa Israeli, amenena neno hili. Zacharie 1.6 Esaïe 1.20 Nombres 23.19 Jérémie 44.29 Psaumes 107.39

Cette Bible est dans le domaine public.