Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 48
Bible en Swahili de l’est


1 Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda; mnaoapa kwa jina la Bwana, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki. Psaumes 68.26 Jérémie 4.2 Esaïe 45.23 Deutéronome 6.13 Esaïe 65.16
2 Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; Bwana wa majeshi ni jina lake. Michée 3.11 Romains 2.17 Esaïe 52.1 Esaïe 10.20 Jérémie 21.2
3 Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; naliyatenda kwa ghafula, yakatokea. Esaïe 41.22 Esaïe 42.9 Esaïe 44.7-44.8 Esaïe 45.21 Josué 21.45
4 Kwa sababu nalijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba; Exode 32.9 Deutéronome 31.27 Actes 7.51 Zacharie 7.11-7.12 Proverbes 29.1
5 basi nimekuonyesha tangu zamani; kabla hayajatukia nalikuonyesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru. Luc 1.70 Esaïe 48.3 Jérémie 44.15-44.18 Esaïe 42.8-42.9 Esaïe 44.7
6 Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonyesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua. Esaïe 42.9 Esaïe 43.8-43.10 Apocalypse 5.1-5.2 Apocalypse 1.19 Psaumes 107.43
7 Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, naliyajua. 8 Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nalijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako; Psaumes 58.3 Esaïe 26.11 Jean 12.39-12.40 Jérémie 5.21 Esaïe 48.4
9 kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali. Psaumes 78.38 Psaumes 103.8-103.10 Esaïe 48.11 Néhémie 9.30-9.31 Esaïe 43.25
10 Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuru ya mateso. Deutéronome 4.20 Jérémie 9.7 Psaumes 66.10 1 Pierre 1.7 Proverbes 17.3
11 Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu. Ezéchiel 20.9 Esaïe 42.8 Deutéronome 32.26-32.27 Esaïe 48.5 Esaïe 37.35
12 Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia. Esaïe 41.4 Apocalypse 22.13 Esaïe 55.3 Apocalypse 1.8 Esaïe 44.6
13 Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja. Esaïe 40.26 Psaumes 102.25 Hébreux 1.10-1.12 Exode 20.11 Esaïe 40.12
14 Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? Bwana amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo. Esaïe 43.9 Esaïe 46.10-46.11 Esaïe 13.4-13.5 Esaïe 13.17-13.18 Jérémie 50.21-50.29
15 Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake. Esaïe 45.1-45.2 Josué 1.8 Ezéchiel 1.2 Psaumes 45.4
16 Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. Esaïe 45.19 Jean 18.20 Jean 20.21-20.22 Esaïe 61.1-61.3 Jean 3.34
17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Psaumes 32.8 Deutéronome 8.17-8.18 Job 22.21-22.22 Psaumes 25.12 Job 36.22
18 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari; Esaïe 66.12 Deutéronome 32.29 Psaumes 119.165 Deutéronome 5.29 Amos 5.24
19 Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu. Esaïe 10.22 Genèse 22.17 Osée 1.10 Jérémie 33.22 Psaumes 109.13
20 Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, Bwana amemkomboa mtumishi wake, Yakobo. Esaïe 52.9 Jérémie 51.6 Zacharie 2.6-2.7 Jérémie 50.8 Jérémie 51.45
21 Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani; Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao; Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu. Exode 17.6 Nombres 20.11 Psaumes 105.41 Esaïe 30.25 Esaïe 43.19-43.20
22 Hapana amani kwa wabaya, asema Bwana. Esaïe 57.21 Job 15.20-15.24 Luc 19.42 Romains 3.17

Cette Bible est dans le domaine public.