Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 55
Bible en Swahili de l’est


1 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani. Jean 7.37-7.38 Apocalypse 21.6 Psaumes 143.6 Cantique 5.1 Esaïe 44.3
2 Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono. Jérémie 31.14 Psaumes 22.26 Osée 8.7 Jean 6.48-6.58 Jérémie 2.13
3 Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara. Jérémie 32.40 Actes 13.34 Psaumes 78.1 Proverbes 4.20 Matthieu 11.28
4 Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu. Daniel 9.25 Jérémie 30.9 Osée 3.5 Ezéchiel 34.23-34.24 Jean 18.37
5 Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya Bwana, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza. Esaïe 60.9 Actes 5.31 Esaïe 52.15 Esaïe 49.6 Genèse 49.10
6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Jérémie 29.12-29.14 Esaïe 45.19 Psaumes 32.6 Amos 5.6 Hébreux 2.3
7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Jacques 4.8-4.10 Esaïe 44.22 Proverbes 28.13 Esaïe 43.25 2 Chroniques 7.14
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Psaumes 92.5 Psaumes 40.5 Ezéchiel 18.29 Osée 14.9 Psaumes 25.10
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Psaumes 103.11 Romains 11.31-11.36 Psaumes 77.19 Psaumes 36.5 Psaumes 89.2
10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; Osée 10.12 Esaïe 30.23 2 Corinthiens 9.9-9.11 Esaïe 61.11 Psaumes 65.9-65.13
11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. Matthieu 24.35 Esaïe 46.10 Jean 6.63 Esaïe 45.23 Romains 10.17
12 Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi. Esaïe 44.23 Esaïe 48.20 Psaumes 105.43 Colossiens 1.11 Esaïe 49.13
13 Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali. Esaïe 41.19 Esaïe 60.13 Jérémie 33.9 Michée 7.4 Esaïe 11.6-11.9

Cette Bible est dans le domaine public.