Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 11
Bible en Swahili de l’est


1 Tena roho ikaniinua, ikanileta hata lango la upande wa mashariki wa nyumba ya Bwana, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu. Ezéchiel 11.24 Ezéchiel 8.16 Ezéchiel 10.19 Ezéchiel 3.12 Ezéchiel 11.13
2 Akaniambia, Mwanadamu, hawa ndio watu wale watungao uovu, na kutoa mashauri mabaya ndani ya mji huu; Esaïe 30.1 Jérémie 5.5 Psaumes 52.2 Psaumes 2.1-2.2 Michée 2.1-2.2
3 wasemao, Wakati wa kujenga nyumba si karibu; mji huu ni sufuria na sisi ni nyama. Ezéchiel 12.22 Ezéchiel 12.27 Jérémie 1.11-1.13 Ezéchiel 7.7 Ezéchiel 11.7-11.11
4 Basi toa unabii juu yao, Ee mwanadamu, toa unabii. Ezéchiel 3.17-3.21 Ezéchiel 3.2-3.15 Ezéchiel 25.2 Osée 6.5 Osée 8.1
5 Roho ya Bwana ikaniangukia, naye akaniambia, Nena, Bwana asema hivi; Mmesema maneno hayo, Enyi nyumba ya Israeli; maana mimi nayajua yaingiayo katika mioyo yenu. Jérémie 17.10 Ezéchiel 2.2 Jérémie 16.17 1 Chroniques 28.9 Actes 10.44
6 Mmewaongeza watu wenu waliouawa ndani ya mji wenu, nanyi mmezijaza njia kuu zake waliouawa. Ezéchiel 7.23 Ezéchiel 22.2-22.6 Ezéchiel 22.27 Ezéchiel 22.9 Esaïe 1.15
7 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Watu wenu waliouawa, ambao mmewalaza katikati yake, hao ndio nyama hiyo, na mji huu ndio sufuria; lakini ninyi mtatolewa nje kutoka katikati yake. Michée 3.2-3.3 Ezéchiel 24.3-24.13 Jérémie 52.24-52.27 2 Rois 25.18-25.22 Ezéchiel 3.9-3.11
8 Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana MUNGU. Proverbes 10.24 Esaïe 66.4 Job 3.25 Esaïe 24.17-24.18 Jean 11.48
9 Nami nitawatoa ninyi nje kutoka katikati yake, na kuwatia katika mikono ya wageni, nami nitafanya hukumu kati yenu. Ezéchiel 5.8 Psaumes 106.41 Deutéronome 28.36 Deutéronome 28.49-28.50 Ezéchiel 16.41
10 Mtaanguka kwa upanga; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 2 Rois 14.25 Jérémie 52.9-52.10 2 Rois 25.19-25.21 Jérémie 39.6 Ezéchiel 6.7
11 Mji huu hautakuwa sufuria lenu, wala ninyi hamtakuwa nyama ndani yake; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; Ezéchiel 11.3 Ezéchiel 11.7-11.10
12 nanyi mtajua ya kuwa mimi ni Bwana; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka. Ezéchiel 8.10 Ezéchiel 8.16 Ezéchiel 8.14 2 Rois 21.2 2 Rois 17.11-17.23
13 Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli? Ezéchiel 11.1 Ezéchiel 9.8 Actes 5.5 Actes 13.11 Josué 7.6-7.9
14 Neno la Bwana likanijia, kusema, 15 Mwanadamu, ndugu zako, naam, ndugu zako, watu wa jamaa zako, na nyumba yote ya Israeli, wote pia, ndio hao ambao wenyeji wa Yerusalemu wamewaambia, Jitengeni mbali na Bwana, nchi hii tumepewa sisi, iwe milki yetu; Ezéchiel 33.24 Esaïe 66.5 Jean 16.2 Jérémie 24.1-24.5 Esaïe 65.5
16 basi nena, Bwana MUNGU asema hivi, Ikiwa mimi nimewahamisha, wakae katika mataifa, na ikiwa mimi nimewatawanya katika nchi kadha wa kadha, pamoja na hayo nitakuwa patakatifu kwao kwa muda mchache, katika nchi zile walizozifikilia. Esaïe 8.14 Psaumes 90.1 Psaumes 31.20 Jérémie 30.11 2 Rois 24.12-24.16
17 Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya kabila za watu, na kuwakutanisha toka nchi zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi ya Israeli. Ezéchiel 28.25 Ezéchiel 34.13 Jérémie 3.18 Jérémie 24.5 Jérémie 3.12
18 Nao watafika huko, nao wataondolea mbali vitu vyake vyote vichukizavyo, na machukizo yake yote. Ezéchiel 37.23 Ezéchiel 5.11 Ezéchiel 7.20 Esaïe 1.25-1.27 Ezéchiel 42.7-42.8
19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama; Ezéchiel 36.26-36.27 Jérémie 31.33 Jérémie 32.39-32.40 Psaumes 51.10 Zacharie 7.12
20 ili waende katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. Ezéchiel 14.11 Psaumes 105.45 Jérémie 30.22 Jérémie 31.33 Hébreux 11.16
21 Bali wao ambao mioyo yao huenda kwa kuufuata moyo wa vitu vyao vichukizavyo, na machukizo yao, nitaileta njia yao iwajilie juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU. Ezéchiel 9.10 Ezéchiel 11.18 Jérémie 29.16-29.19 Jérémie 1.16 Ezéchiel 20.38
22 Ndipo hao makerubi wakainua mabawa yao, nayo magurudumu yalikuwa karibu nao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. Ezéchiel 10.19 Ezéchiel 1.19-1.20
23 Utukufu wa Bwana ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji. Zacharie 14.4 Ezéchiel 8.4 Ezéchiel 10.4 Ezéchiel 43.2 Ezéchiel 10.18
24 Na roho hiyo ikaniinua, ikanichukua katika maono, kwa nguvu za roho ya Mungu, hata Ukaldayo, kwa watu wale wa uhamisho. Basi maono niliyoyaona yakaniacha. Ezéchiel 11.1 Ezéchiel 8.3 Ezéchiel 1.3 Actes 10.16 Ezéchiel 3.12
25 Ndipo nikawaambia watu wa uhamisho habari ya mambo yote aliyonionyesha Bwana. Ezéchiel 3.4 Ezéchiel 2.7 Ezéchiel 3.27 Ezéchiel 3.17

Cette Bible est dans le domaine public.