Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 7
Bible en Swahili de l’est


1 Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwivi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang’anyi hushambulia nje. Osée 4.2 Osée 6.4 Osée 11.12-12.1 Osée 7.13 Osée 6.8-6.10
2 Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu. Psaumes 90.8 Jérémie 2.19 Jérémie 14.10 Amos 8.7 Psaumes 25.7
3 Humfurahisha mfalme kwa uovu wao, na wakuu wao kwa uongo wao. Romains 1.32 Michée 7.3 Jérémie 28.1-28.4 Amos 7.10-7.13 1 Rois 22.13
4 Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuu iliyotiwa moto na mwokaji; huacha kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hata umekwisha kutiwa chachu. Jérémie 9.2 Jérémie 5.7-5.8 Osée 7.6-7.7 Osée 4.2 Osée 4.12
5 Sikukuu ya mfalme wetu, wakuu walijitapisha kwa ukali wa divai; alinyosha mkono wake pamoja na wenye mzaha. Esaïe 28.1 Genèse 40.20 Esaïe 28.7-28.8 Esaïe 5.11-5.12 Proverbes 13.20
6 Maana wamefanya moyo wao kuwa tayari kama tanuu, wakati waoteapo; hasira yao hulala usiku kucha; asubuhi yawaka kama moto utoao miali. Psaumes 21.9 Psaumes 10.8-10.9 Proverbes 4.16 Osée 7.4 2 Samuel 13.28-13.29
7 Wote wamepata moto kama tanuu, nao hula makadhi wao; wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao aniitaye mimi. 2 Rois 15.30 2 Rois 15.14 2 Rois 15.25 2 Rois 15.10 Esaïe 43.22
8 Efraimu ajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa. Psaumes 106.35 Osée 5.13 Osée 8.2-8.4 Matthieu 6.24 1 Rois 18.21
9 Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari. Osée 8.7 2 Rois 13.3-13.7 Proverbes 23.35 Esaïe 57.1 Esaïe 42.22-42.25
10 Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote. Osée 5.5 Esaïe 9.13 Amos 4.6-4.13 Osée 7.7 Jérémie 35.15-35.17
11 Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru. Osée 5.13 Osée 12.1 Osée 11.11 Osée 4.11 Osée 9.3
12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia. Ezéchiel 12.13 Deutéronome 28.15-28.68 Ezéchiel 17.20 Apocalypse 3.19 2 Rois 17.13-17.18
13 Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu. Osée 9.12 Osée 11.12 Jérémie 18.11-18.12 Esaïe 43.1 Esaïe 59.13
14 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi. Amos 2.8 Jérémie 3.10 Job 35.9-35.10 Michée 2.11 Zacharie 7.5
15 Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu. Nahum 1.9 Proverbes 3.11 Apocalypse 3.19 Psaumes 94.12 Romains 1.21
16 Wao hurudi, lakini si kwake Aliye juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya jeuri ya ndimi zao; jambo hili litakuwa kwao sababu ya kuchekwa katika nchi ya Misri. Psaumes 78.57 Osée 9.3 Psaumes 73.9 Ezéchiel 23.32 Psaumes 12.4

Cette Bible est dans le domaine public.