Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 7.7
Bible en Swahili de l’est


1 Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwivi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang’anyi hushambulia nje.Osée 6.4 Osée 4.2 Esaïe 59.12 Michée 7.3-7.7 Jérémie 51.9
2 Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.Psaumes 90.8 Jérémie 2.19 Jérémie 14.10 Hébreux 4.13 Jérémie 4.18
3 Humfurahisha mfalme kwa uovu wao, na wakuu wao kwa uongo wao.Romains 1.32 Michée 7.3 Jérémie 28.1-28.4 Jérémie 5.31 Michée 6.16
4 Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuu iliyotiwa moto na mwokaji; huacha kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hata umekwisha kutiwa chachu.Jérémie 9.2 Jacques 4.4 Jérémie 5.7-5.8 Osée 7.6-7.7 Osée 4.2
5 Sikukuu ya mfalme wetu, wakuu walijitapisha kwa ukali wa divai; alinyosha mkono wake pamoja na wenye mzaha.Esaïe 28.1 1 Rois 13.4 Psaumes 69.12 Esaïe 5.22-5.23 Proverbes 20.1
6 Maana wamefanya moyo wao kuwa tayari kama tanuu, wakati waoteapo; hasira yao hulala usiku kucha; asubuhi yawaka kama moto utoao miali.Michée 2.1 1 Samuel 19.11-19.15 Psaumes 21.9 Psaumes 10.8-10.9 Proverbes 4.16
7 Wote wamepata moto kama tanuu, nao hula makadhi wao; wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao aniitaye mimi.2 Rois 15.14 2 Rois 15.25 2 Rois 15.10 2 Rois 15.30 Esaïe 64.7
8 Efraimu ajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa.Psaumes 106.35 Osée 5.13 Sophonie 1.5 Néhémie 13.23-13.25 Osée 5.7
9 Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari.Osée 8.7 2 Rois 15.19 2 Rois 13.3-13.7 Proverbes 23.35 Esaïe 57.1
10 Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.Osée 5.5 Esaïe 9.13 Amos 4.6-4.13 Proverbes 27.22 Romains 3.11
11 Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru.Osée 5.13 Osée 12.1 Osée 4.11 Osée 11.11 Osée 9.3
12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.Ezéchiel 12.13 Deutéronome 28.15-28.68 Ecclésiaste 9.12 Job 19.6 Jérémie 16.16
13 Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.Osée 9.12 Osée 11.12 Apocalypse 8.13 Deutéronome 15.15 Psaumes 106.10
14 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.Amos 2.8 Job 35.9-35.10 Michée 2.11 Zacharie 7.5 Juges 9.27
15 Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu.Nahum 1.9 2 Rois 13.5 2 Rois 14.25-14.27 Hébreux 12.5 Jérémie 17.9
16 Wao hurudi, lakini si kwake Aliye juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya jeuri ya ndimi zao; jambo hili litakuwa kwao sababu ya kuchekwa katika nchi ya Misri.Psaumes 78.57 Osée 9.3 Ezéchiel 23.32 Psaumes 73.9 Psaumes 12.4

Cette Bible est dans le domaine public.