Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 7.9
Bible en Swahili de l’est


1 Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwivi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang’anyi hushambulia nje.Osée 6.4 Osée 4.2 Matthieu 23.37 Osée 8.9 Osée 5.1
2 Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.Psaumes 90.8 Jérémie 2.19 Jérémie 14.10 1 Corinthiens 4.5 Osée 9.9
3 Humfurahisha mfalme kwa uovu wao, na wakuu wao kwa uongo wao.Michée 7.3 Romains 1.32 Jérémie 28.1-28.4 Osée 7.5 Amos 7.10-7.13
4 Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuu iliyotiwa moto na mwokaji; huacha kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hata umekwisha kutiwa chachu.Jérémie 9.2 Jacques 4.4 Jérémie 5.7-5.8 Osée 7.6-7.7 Osée 4.2
5 Sikukuu ya mfalme wetu, wakuu walijitapisha kwa ukali wa divai; alinyosha mkono wake pamoja na wenye mzaha.Esaïe 28.1 Matthieu 14.6 Ephésiens 5.18 Marc 6.21 Habakuk 2.15-2.16
6 Maana wamefanya moyo wao kuwa tayari kama tanuu, wakati waoteapo; hasira yao hulala usiku kucha; asubuhi yawaka kama moto utoao miali.Michée 2.1 1 Samuel 19.11-19.15 Psaumes 21.9 Psaumes 10.8-10.9 Proverbes 4.16
7 Wote wamepata moto kama tanuu, nao hula makadhi wao; wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao aniitaye mimi.2 Rois 15.25 2 Rois 15.10 2 Rois 15.30 2 Rois 15.14 Osée 7.10
8 Efraimu ajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa.Psaumes 106.35 Osée 5.13 Apocalypse 3.15-3.16 Esdras 9.1 Osée 8.2-8.4
9 Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari.Osée 8.7 2 Rois 15.19 2 Rois 13.3-13.7 Proverbes 23.35 Esaïe 57.1
10 Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.Osée 5.5 Esaïe 9.13 Amos 4.6-4.13 Jérémie 3.3 Osée 6.1
11 Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru.Osée 5.13 Osée 12.1 Osée 11.11 Osée 4.11 Osée 9.3
12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.Ezéchiel 12.13 Deutéronome 28.15-28.68 Jérémie 44.4 Deutéronome 32.15-32.43 Ezéchiel 17.20
13 Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.Osée 9.12 Osée 11.12 Jonas 1.3 Job 22.17 Job 21.14-21.15
14 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.Amos 2.8 Michée 2.11 Zacharie 7.5 Juges 9.27 Jérémie 3.10
15 Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu.Nahum 1.9 2 Rois 13.23 Job 5.17 2 Corinthiens 10.5 Actes 4.25
16 Wao hurudi, lakini si kwake Aliye juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya jeuri ya ndimi zao; jambo hili litakuwa kwao sababu ya kuchekwa katika nchi ya Misri.Psaumes 78.57 Osée 9.3 Psaumes 73.9 Ezéchiel 23.32 Osée 9.6

Cette Bible est dans le domaine public.