Naissance et règne du Messie
1 Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Lamentations 3.30 Job 16.10 Esaïe 33.22 Jérémie 25.9 Luc 19.43-19.44
2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Matthieu 2.6 Jean 7.42 Esaïe 11.1 Luc 1.31-1.33 Zacharie 9.9
3 Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.
Osée 11.8 Michée 7.13 Esaïe 10.20-10.21 Michée 4.7 Michée 4.9-4.10
4 Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.
Michée 7.14 Luc 1.32 Esaïe 52.10 Zacharie 9.10 Psaumes 72.8
5 Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mtaondokesha wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane.
Luc 2.14 Zacharie 9.10 Amos 1.3 Job 5.19 Zacharie 1.18-1.21
6 Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.Genèse 10.8-10.11 Esaïe 14.25 Luc 1.74 Esaïe 14.2 2 Rois 17.3-17.5
7 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.
Deutéronome 32.2 Michée 5.3 Psaumes 110.3 Psaumes 72.6 Osée 14.5
8 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa.
Zacharie 10.5 Michée 4.13 Psaumes 50.22 Osée 5.14 Esaïe 41.15-41.16
9 Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.
Esaïe 26.11 Psaumes 21.8 Esaïe 11.14 Apocalypse 20.8-20.9 1 Corinthiens 15.25
10 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;
Zacharie 9.10 Osée 14.3 Psaumes 20.7-20.8 Osée 1.7 Esaïe 2.7
11 nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha;
Esaïe 2.12-2.17 Amos 5.9 Ezéchiel 38.11 Osée 10.14 Esaïe 6.11
12 nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;
Deutéronome 18.10-18.12 Apocalypse 19.20 Esaïe 2.6-2.8 Esaïe 2.20 Apocalypse 22.15
13 nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.
Ezéchiel 6.9 Osée 14.3 Esaïe 2.8 Osée 2.16-2.17 Esaïe 17.7-17.8
14 Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.
Exode 34.13
15 Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.
Michée 5.8 Psaumes 149.7 2 Thessaloniciens 1.8 Esaïe 65.12