Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Malachie 3
Bible en Swahili de l’est


1 Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Malachie 4.5 Luc 1.76 Esaïe 63.9 Jean 1.6-1.7 Actes 19.4
2 Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Zacharie 13.9 1 Corinthiens 3.13-3.15 Esaïe 4.4 Apocalypse 6.17 Psaumes 2.7
3 naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Esaïe 1.25 Daniel 12.10 Luc 3.16 Jean 4.23-4.24 Tite 2.14
4 Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. 2 Chroniques 7.1-7.3 2 Chroniques 8.12-8.14 Jérémie 31.23-31.24 Ezéchiel 20.40-20.41 Jérémie 30.18-30.20
5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi. Lévitique 19.13 Jérémie 29.23 Deutéronome 24.17 Deutéronome 27.19 Malachie 2.14
6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Nombres 23.19 Lamentations 3.22-3.23 Jacques 1.17 Hébreux 13.8 Apocalypse 1.8
7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? Zacharie 1.3 Deutéronome 31.20 Deutéronome 30.1-30.4 Ezéchiel 20.21 1 Rois 8.47-8.49
8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Romains 13.7 Proverbes 3.9-3.10 Matthieu 22.21 Nombres 18.21-18.32 Marc 12.17
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Malachie 2.2 Aggée 2.14-2.17 Deutéronome 28.15-28.19 Aggée 1.6-1.11 Josué 22.20
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Proverbes 3.9-3.10 Matthieu 6.33 2 Corinthiens 9.6-9.8 Néhémie 13.10-13.13 Psaumes 37.3
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Amos 7.1-7.3 Amos 4.9 Aggée 2.17 Joël 2.22 Zacharie 8.12
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. Esaïe 61.9 Zacharie 8.23 Esaïe 62.4 Jérémie 33.9 Deutéronome 8.7-8.10
13 Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? Malachie 2.17 Jérémie 8.12 Psaumes 10.11 Esaïe 37.23 Malachie 2.14
14 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? Esaïe 58.3 Sophonie 1.12 Psaumes 73.8-73.13 Job 21.14-21.15 Job 22.17
15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. Malachie 4.1 Jérémie 7.10 Ecclésiaste 9.1-9.2 Daniel 5.20-5.28 Daniel 4.37
16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. Psaumes 56.8 Apocalypse 20.12 Malachie 3.5 Psaumes 119.63 2 Samuel 7.1
17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. Exode 19.5 Deutéronome 7.6 Esaïe 62.3-62.4 2 Corinthiens 6.18 Jérémie 32.38-32.39
18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia. Genèse 18.25 Psaumes 58.10-58.11 Malachie 3.14-3.15 Josué 24.15 Jérémie 12.15

Cette Bible est dans le domaine public.