Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 36
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha wale wakuu wa nyumba za mababa ya jamaa ya wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, katika jamaa za wana wa Yusufu, wakakaribia, na kunena mbele ya Musa, na mbele ya wakuu walio juu ya nyumba za mababa ya wana wa Israeli; Nombres 27.1 1 Chroniques 7.14-7.16 Josué 17.2-17.3 Nombres 26.29-26.33
2 wakasema, Bwana alimwagiza bwana wangu awape wana wa Israeli nchi kwa kupiga kura iwe urithi wao; tena bwana wangu aliagizwa na Bwana awape binti za Selofehadi ndugu yetu huo urithi wa baba yao. Nombres 33.54 Nombres 27.1-27.7 Nombres 26.55-26.56 Job 42.15 Josué 17.3-17.6
3 Wakiolewa na watu wa wana wa hizo kabila nyingine za wana wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba zetu, na hiyo kabila watakayotiwa ndani yake itaongezewa urithi wao; basi urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu. 4 Tena itakapokuwapo hiyo yubile ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hiyo kabila ambayo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila ya baba zetu. Luc 4.18-4.19 Lévitique 25.23 Lévitique 25.10-25.18 Esaïe 61.2
5 Basi Musa akawaagiza wana wa Israeli kama neno la Bwana lilivyokuwa, akasema, Kabila ya wana wa Yusufu imenena yaliyo haki. Nombres 27.7 Deutéronome 5.28
6 Bwana ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila ya baba zao. Genèse 24.57-24.58 Nombres 36.12 2 Corinthiens 6.14 Genèse 24.3
7 Hivyo hapana urithi wo wote wa wana wa Israeli utakaotoka kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu na urithi wa kabila ya baba zake. 1 Rois 21.3 Nombres 36.9
8 Na kila binti atakayemiliki urithi katika kabila yo yote katika wana wa Israeli, ataolewa katika jamaa moja ya kabila ya baba yake, ili wana wa Israeli wapate kumiliki kila mtu urithi wa baba zake. 1 Chroniques 23.22
9 Hivyo hapatakuwa na urithi uwao wote utakaotoka kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa kabila za wana wa Israeli zitashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe. 10 Basi hao binti za Selofehadi wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa; Matthieu 28.20 Lévitique 24.23 2 Chroniques 30.12 Exode 39.42-39.43
11 kwa kuwa Mala, na Tirsa, na Hogla, na Milka, na Noa, binti za Selofehadi waliolewa na waume, wana wa ndugu za baba yao. Nombres 27.1 Nombres 26.33
12 Waliolewa katika jamaa za wana wa Manase, mwana wa Yusufu, na urithi wao ukakaa katika kabila ya jamaa ya baba yao. 13 Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo Bwana aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko Lévitique 27.34 Nombres 22.1 Nombres 33.50 Lévitique 14.54-14.57 Nombres 35.1

Cette Bible est dans le domaine public.