Sur les viandes sacrifiées aux idoles
1 Na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga.
1 Corinthiens 8.7 1 Corinthiens 8.4 Romains 14.3 Esaïe 5.21 Romains 15.14
2 Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.
1 Corinthiens 13.12 1 Corinthiens 3.18 1 Timothée 6.3-6.4 1 Corinthiens 13.8-13.9 Galates 6.3
3 Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejulikana naye.
Apocalypse 3.8-3.9 Galates 4.9 Exode 33.17 Apocalypse 2.19 Nahum 1.7
4 Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.
Deutéronome 6.4 Deutéronome 4.39 Esaïe 41.24 1 Timothée 2.5 Esaïe 44.6
5 Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi;
2 Thessaloniciens 2.4 Deutéronome 10.17 Jérémie 11.13 Galates 4.8 Jérémie 2.11
6 lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.
Jean 1.3 Ephésiens 4.5-4.6 Malachie 2.10 Romains 11.36 1 Corinthiens 8.4
7 Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote; ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa hula kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.
Romains 14.14 1 Corinthiens 10.28-10.29 1 Corinthiens 8.9-8.10 Romains 14.22-14.23 1 Corinthiens 1.10-1.11
8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.
Romains 14.17 1 Corinthiens 6.13 Colossiens 2.20-2.23 Hébreux 13.9
9 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.
Galates 5.13 Romains 14.20-14.21 Romains 14.13-14.15 1 Corinthiens 10.24 Romains 14.1-14.2
10 Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?Juges 9.27 1 Corinthiens 10.32 Nombres 25.2 Romains 14.23 1 Corinthiens 8.4
11 Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
Romains 14.15 1 Corinthiens 8.13 Romains 14.20-14.21 1 Corinthiens 10.33-11.1 Romains 15.1-15.3
12 Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo.
Matthieu 25.45 Matthieu 18.6 1 Samuel 19.4-19.5 1 Samuel 2.25 Matthieu 18.21
13 Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.
Romains 14.21 2 Corinthiens 11.29 1 Corinthiens 13.5 2 Corinthiens 6.3 1 Corinthiens 9.19-9.23