Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Timothée 3.6
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.2 Pierre 3.3 1 Timothée 4.1-4.3 2 Timothée 4.3 Ezéchiel 38.16 Michée 4.1
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,Jude 1.16 Philippiens 2.21 Psaumes 10.3 2 Pierre 2.12 Jacques 4.16
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,Romains 1.31 1 Timothée 3.11 Genèse 49.7 Esaïe 53.3 Apocalypse 17.6
4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;1 Timothée 3.6 Philippiens 3.18-3.19 Jude 1.19 2 Pierre 2.10-2.22 Romains 16.18
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.Matthieu 23.27-23.28 Romains 2.20-2.24 Esaïe 29.13 Ezéchiel 33.30-33.32 Matthieu 7.15
6 Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;Jude 1.4 Tite 1.11 Tite 3.3 Jude 1.18 1 Corinthiens 12.2
7 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.Esaïe 30.10-30.11 2 Timothée 2.25 1 Corinthiens 3.1-3.4 Hébreux 5.11 Matthieu 13.11
8 Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.Exode 7.11 1 Timothée 6.5 Tite 1.16 Actes 13.8-13.11 Galates 2.4-2.5
9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.Exode 7.12 Exode 9.11 Exode 8.18-8.19 1 Rois 22.25 Jérémie 29.31-29.32
10 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,Philippiens 2.22 1 Timothée 4.6 1 Timothée 6.11 Tite 2.7 2 Corinthiens 6.4-6.10
11 na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.Actes 13.45 Actes 14.5-14.6 Psaumes 34.19 Actes 13.14 2 Corinthiens 11.23-11.28
12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.Actes 14.22 1 Pierre 2.20-2.21 1 Pierre 4.12-4.16 1 Corinthiens 15.19 Tite 2.12
13 lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.2 Pierre 2.20 Tite 3.3 2 Timothée 3.8 1 Timothée 4.1 Ezéchiel 14.9-14.10
14 Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;2 Timothée 1.13 1 Thessaloniciens 2.13 2 Timothée 2.2 1 Thessaloniciens 1.5 Romains 14.5
15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.2 Timothée 1.5 2 Pierre 1.20-1.21 Psaumes 119.98-119.99 Luc 24.45 Matthieu 22.29
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;Romains 15.4 Hébreux 4.12 2 Pierre 1.19-1.21 Marc 12.24 Psaumes 19.7-19.11
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.2 Timothée 2.21 1 Timothée 6.11 Hébreux 10.24 2 Corinthiens 9.8 Néhémie 2.18

Cette Bible est dans le domaine public.