Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jacques 4.2
Bible en Swahili de l’est


1 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?Romains 7.23 1 Pierre 2.11 Galates 5.17 Jacques 1.14 Jacques 4.3
2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!Jean 16.24 Jacques 1.5 Matthieu 7.7-7.8 1 Timothée 6.9-6.10 Jacques 5.1-5.5
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.1 Jean 5.14 1 Jean 3.22 Psaumes 18.41 Proverbes 21.13 Psaumes 66.18-66.19
4 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.Jean 15.19 1 Jean 2.15-2.16 Romains 8.7 Matthieu 6.24 Galates 1.10
5 Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?1 Corinthiens 6.19 2 Corinthiens 6.16 Nombres 11.29 Genèse 6.5
6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.Matthieu 23.12 Proverbes 3.34 Psaumes 138.6 1 Pierre 5.5 Proverbes 18.12
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.1 Pierre 5.8-5.9 Ephésiens 4.27 Ephésiens 6.11-6.12 1 Pierre 5.6 Hébreux 12.9
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.Zacharie 1.3 2 Chroniques 15.2 Malachie 3.7 Psaumes 145.18 Esaïe 55.6-55.7
9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.Luc 6.25 Matthieu 5.4 Proverbes 14.13 Jérémie 31.18-31.20 Jacques 5.1-5.2
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.Matthieu 23.12 Luc 14.11 1 Pierre 5.6 Job 22.29 Psaumes 113.7
11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.1 Pierre 2.1 Psaumes 140.11 Romains 2.1 Jacques 5.9 Matthieu 7.1-7.2
12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?Romains 14.4 Matthieu 10.28 Esaïe 33.22 Romains 2.1 Romains 9.20
13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;Proverbes 27.1 Luc 12.17-12.20 Jacques 5.1 Genèse 11.3-11.4 Esaïe 56.11-56.12
14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.Psaumes 102.3 1 Pierre 1.24 Psaumes 39.5 Job 14.1-14.2 Job 7.6-7.7
15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.Actes 18.21 Proverbes 19.21 Hébreux 6.3 Lamentations 3.37 1 Corinthiens 4.19
16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.1 Corinthiens 5.6 Proverbes 25.14 Psaumes 52.1 Psaumes 52.7 Proverbes 27.1
17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.Jean 9.41 Jean 15.22 Jean 13.17 2 Pierre 2.21 Romains 1.32

Cette Bible est dans le domaine public.