Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Samuel 27.11
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kwa habari yangu, asinitafute tena mipakani mwote mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake.Esaïe 30.15-30.16 2 Corinthiens 7.5 Nombres 14.3 Matthieu 14.31 1 Samuel 22.5
2 Basi Daudi akaondoka, yeye na hao watu mia sita aliokuwa nao, akamvukia Akishi, mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.1 Samuel 21.10 1 Samuel 25.13 1 Samuel 30.8 1 Rois 2.39-2.40
3 Daudi akakaa huko Gathi pamoja na Akishi, yeye na watu wake, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; Daudi naye alikuwa na wakeze wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, aliyekuwa mkewe Nabali.1 Samuel 25.42-25.43 1 Samuel 25.3 1 Samuel 25.18-25.35 1 Samuel 30.5 1 Samuel 30.3
4 Naye Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia mpaka Gathi; wala hakumtafuta tena.1 Samuel 26.21
5 Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?2 Corinthiens 6.17 Genèse 46.34
6 Ndipo Akishi akampa Siklagi siku ile; kwa sababu hiyo huo mji wa Siklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hata hivi leo.Néhémie 11.28 Josué 15.31 1 Samuel 30.1 2 Samuel 1.1 1 Samuel 30.14
7 Na hesabu ya siku alizokaa Daudi katika nchi ya Wafilisti ilikuwa mwaka mzima na miezi minne.1 Samuel 29.3
8 Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, hata mpaka nchi ya Misri.1 Samuel 15.7-15.8 Josué 13.2 Josué 13.13 Josué 16.10 Juges 1.29
9 Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng’ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi.1 Samuel 15.3 Deutéronome 25.17-25.19 Genèse 16.7 1 Samuel 15.7 Genèse 25.18
10 Naye Akishi humwuliza, Je! Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi husema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni.Juges 1.16 1 Chroniques 2.9 1 Chroniques 2.25 Juges 4.11 1 Samuel 30.29
11 Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.Proverbes 29.25 1 Samuel 22.22 Proverbes 12.19
12 Hivyo Akishi akamsadiki Daudi, akasema, Amewachukiza kabisa hao watu wake Israeli; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu hata milele.Genèse 34.30 1 Samuel 13.4

Cette Bible est dans le domaine public.