Mort de Saül et de Jonathan
1 Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima wa Gilboa.
1 Samuel 28.4 1 Chroniques 10.1-10.12 2 Samuel 1.21 1 Samuel 28.1 1 Samuel 29.1
2 Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli.
1 Chroniques 8.33 1 Samuel 14.49 Exode 20.5 1 Samuel 18.1-18.4 1 Chroniques 9.39
3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde.
2 Samuel 1.6 Amos 2.14 Genèse 49.23 1 Rois 22.34 2 Samuel 1.4
4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
Juges 9.54 1 Samuel 14.6 1 Samuel 17.36 2 Samuel 1.14 2 Samuel 17.23
5 Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye.
1 Chroniques 10.5
6 Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo.
1 Samuel 12.25 Ecclésiaste 9.1-9.2 1 Samuel 11.15 Osée 13.10-13.11 1 Chroniques 10.6
7 Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng’ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
Lévitique 26.36 Deutéronome 28.33 1 Samuel 13.6 Lévitique 26.32 Juges 6.2
8 Hata ikawa, siku ya pili yake, Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara waliouawa, walimwona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.1 Chroniques 10.8 2 Chroniques 20.25
9 Wakamkata kichwa, wakamvua silaha zake, wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari nyumbani mwa sanamu zao, na kwa watu.
2 Samuel 1.20 Juges 16.23-16.24 1 Samuel 31.4 1 Chroniques 10.9-10.10 1 Samuel 17.51
10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa Maashtorethi; wakakitundika kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-shani.
Juges 2.13 Josué 17.11 1 Samuel 21.9 1 Samuel 7.3 Juges 1.27
11 Na wenyeji wa Yabesh-Gileadi waliposikia habari zake, jinsi hao Wafilisti walivyomtenda Sauli,
2 Samuel 2.4 1 Samuel 11.1-11.11
12 wakainuka mashujaa wote, wakaenda usiku kucha, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, na kuiondoa ukutani kwa Beth-shani nao wakaja Yabeshi, na kuiteketeza huko.
2 Chroniques 16.14 2 Samuel 2.4-2.7 Amos 6.10 Jérémie 34.5
13 Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.
2 Samuel 21.12-21.14 Genèse 50.10 1 Samuel 22.6 2 Samuel 1.12 Genèse 35.8