Invasion de Juda
1 Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha torati ya Bwana, na Israeli wote pamoja naye.
2 Chroniques 11.17 2 Chroniques 12.13 2 Chroniques 26.13-26.16 1 Rois 14.22-14.24 Deutéronome 32.15
2 Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi Bwana;
1 Rois 11.40 Esaïe 63.10 Jérémie 2.19 2 Chroniques 7.19-7.20 Néhémie 9.26-9.27
3 mwenye magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi sitini elfu; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.
2 Chroniques 16.8 Nahum 3.9 Daniel 11.43 Juges 6.5 Apocalypse 9.16
4 Akaitwaa miji yenye maboma iliyokuwa ya Yuda, akaja Yerusalemu.
2 Chroniques 11.5-11.12 2 Rois 18.17 Jérémie 5.10 Esaïe 8.8 Esaïe 36.1
5 Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, Bwana asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.
2 Chroniques 15.2 2 Chroniques 11.2 1 Rois 12.22 Juges 10.9-10.14 Jérémie 5.19
6 Ndipo wakajinyenyekeza wakuu wa Israeli na mfalme; wakasema, Bwana ndiye mwenye haki.
Exode 9.27 Daniel 9.14 Lamentations 1.18 Job 33.27 2 Chroniques 32.26
7 Naye Bwana alipoona ya kwamba wamejinyenyekeza, neno la Bwana likamjia Shemaya, kusema, Wamejinyenyekeza; sitawaharibu; lakini nitawapa wokovu punde, wala ghadhabu yangu haitamwagika juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.
2 Chroniques 34.25 Apocalypse 16.2-16.17 Esaïe 42.25 Jérémie 7.20 Psaumes 79.6
8 Walakini watamtumikia; ili wapate kujua utumwa wangu, na huo utumwa wa falme za nchi.
Deutéronome 28.47-28.48 Esaïe 26.13 Juges 3.1 Jérémie 10.24 Osée 8.10
9 Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani.
2 Chroniques 9.15-9.16 1 Rois 10.16-10.17 1 Rois 15.18 2 Rois 16.8 2 Rois 18.15-18.16
10 Mfalme Rehoboamu akafanya ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme.
2 Samuel 8.18 1 Chroniques 11.25 2 Samuel 23.23 Lamentations 4.1 Cantique 3.7-3.8
11 Ikawa kila wakati mfalme alipoingia nyumbani mwa Bwana, wakaja walinzi wakazichukua, wakazirudisha tena chumbani mwa walinzi.
12 Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya Bwana ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema.
2 Chroniques 19.3 2 Chroniques 12.6-12.7 1 Rois 14.13 2 Chroniques 33.12-33.13 Lamentations 3.33
13 Basi mfalme Rehoboamu akajitia nguvu katika Yerusalemu, akatawala; maana Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji aliouchagua Bwana miongoni mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke huko jina lake. Na jina la mamaye aliitwa Naama Mwamoni.
1 Rois 14.21 Deutéronome 12.5 2 Chroniques 6.6 Deutéronome 23.3 Néhémie 13.1
14 Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute Bwana.
2 Chroniques 19.3 Psaumes 78.37 Esaïe 55.6-55.7 Matthieu 7.7 Esaïe 45.19
15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
2 Chroniques 9.29 2 Chroniques 12.5 2 Chroniques 13.22 1 Rois 12.22 1 Rois 14.29-14.30
16 Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.
1 Chroniques 3.10 2 Chroniques 11.20 1 Rois 14.29-14.31 Matthieu 1.7 2 Chroniques 13.1