Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 7.13
Bible en Swahili de l’est


1 Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?Job 14.5-14.6 Psaumes 39.4 Job 14.13-14.14 Deutéronome 15.18 Job 5.7
2 Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake;Lévitique 19.13 Jérémie 6.4 Deutéronome 24.15 Jacques 5.4 Malachie 3.5
3 Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha.Psaumes 6.6 Ecclésiaste 1.14 Job 16.7 Psaumes 39.5 Job 29.2
4 Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.Deutéronome 28.67 Job 7.13-7.14 Job 17.12 Psaumes 130.6 Esaïe 54.11
5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.Esaïe 14.11 Job 17.14 Job 2.7-2.8 Job 30.18-30.19 Job 9.31
6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.Job 9.25 Job 17.15 Esaïe 38.12-38.13 1 Pierre 1.24 Job 17.11
7 Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.Psaumes 78.39 Jacques 4.14 Psaumes 89.50 Psaumes 74.22 Psaumes 74.18
8 Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena; Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.Job 20.9 Psaumes 37.36 Job 8.18 Job 13.27 Psaumes 39.11
9 Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.2 Samuel 12.23 Job 30.15 Job 10.21 Job 16.22 Job 14.10-14.14
10 Hatarudi tena nyumbani kwake, Wala mahali pake hapatamjua tena.Job 8.18 Psaumes 103.16 Job 20.9 Job 27.23 Job 27.21
11 Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.Psaumes 40.9 1 Samuel 1.10 Job 10.1 Job 21.25 Esaïe 38.15
12 Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi? Hata ukawaweka walinzi juu yangu?Job 38.6-38.11 Ezéchiel 32.2-32.3 Job 41.1-41.34 Lamentations 3.7 Job 7.17
13 Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo, Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;Psaumes 6.6 Job 9.27-9.28 Job 7.3-7.4 Psaumes 77.4
14 Ndipo unitishapo kwa ndoto, Na kunitia hofu kwa maono;Daniel 2.1 Genèse 41.8 Juges 7.13-7.14 Matthieu 27.19 Genèse 40.5-40.7
15 Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa, Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.2 Samuel 17.23 Matthieu 27.5
16 Ninadhoofika; sitaishi sikuzote; Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.Job 10.1 1 Rois 19.4 Job 14.6 Job 9.21 Psaumes 39.13
17 Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza, Na kumtia moyoni mwako,Hébreux 2.6 Psaumes 8.4 Psaumes 144.3 1 Samuel 24.14 Job 34.14-34.15
18 Na kumwangalia kila asubuhi, Na kumjaribu kila dakika?1 Pierre 1.7 Jérémie 9.7 Esaïe 26.14 Zacharie 13.9 Exode 20.5
19 Je! Hata lini hukomi kuniangalia; Wala kunisumbua hata nimeze mate?Job 9.18 Job 14.6 Psaumes 94.3 Psaumes 13.1-13.3 Apocalypse 6.10
20 Kwamba nimefanya dhambi, nikufanyieje Ee mlinda wanadamu? Mbona umeniweka niwe shabaha yako, Hata nimekuwa mzigo kwa nafsi yangu?Lamentations 3.12 Psaumes 36.6 Job 22.5 Job 6.4 Job 7.11-7.12
21 Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.Job 10.14 Daniel 12.2 Tite 2.14 Jean 1.29 Job 21.32-21.33

Cette Bible est dans le domaine public.