Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 144
Bible en Swahili de l’est


1 Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana. Psaumes 18.34 Psaumes 18.2 2 Samuel 22.35 2 Corinthiens 10.4 Deutéronome 32.30-32.31
2 Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu. Psaumes 18.2 Psaumes 91.2 Psaumes 59.9 2 Samuel 22.2-22.3 Psaumes 18.47
3 Ee Bwana, mtu ni kitu gani hata umjue? Na binadamu hata umwangalie? Psaumes 8.4 Hébreux 2.6 Job 7.17 Job 15.14 Psaumes 146.3-146.4
4 Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho. Psaumes 102.11 Psaumes 109.23 Job 8.9 Psaumes 89.47 Ecclésiaste 12.8
5 Bwana, uziinamishe mbingu zako, ushuke, Uiguse milima nayo itatoka moshi. Psaumes 104.32 Psaumes 18.9 Esaïe 64.1-64.2 Nahum 1.3-1.6 Habakuk 3.3-3.6
6 Utupe umeme, uwatawanye, Uipige mishale yako, uwafadhaishe. Deutéronome 32.23 2 Samuel 22.12-22.15 Psaumes 21.12 Psaumes 77.17-77.18 Deutéronome 32.42
7 Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye, Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni. Psaumes 18.16 Psaumes 69.1-69.2 Psaumes 18.44 Psaumes 93.3-93.4 Apocalypse 17.15
8 Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo. Psaumes 12.2 Psaumes 41.6 Esaïe 44.20 Psaumes 106.26 Psaumes 109.2-109.3
9 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia. Psaumes 33.2-33.3 Psaumes 40.3 Psaumes 81.1-81.3 Psaumes 98.1 1 Chroniques 25.1-25.6
10 Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu. Psaumes 18.50 Psaumes 140.7 Psaumes 33.16-33.18 2 Samuel 5.19-5.25 2 Samuel 8.6-8.14
11 Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo. Psaumes 12.2 Psaumes 144.7-144.8 2 Samuel 17.1-17.14 Esaïe 44.20 2 Samuel 16.5-16.14
12 Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu. Psaumes 128.3 Proverbes 31.10-31.27 Esaïe 3.16-3.24 Lamentations 4.2 Esaïe 44.3-44.5
13 Ghala zetu na zijae Zenye akiba za jinsi zote. Kondoo zetu na wazae Elfu na makumi elfu mashambani mwetu. Deutéronome 7.13-7.14 Deutéronome 8.3 Luc 12.16-12.20 Malachie 3.10 Lévitique 26.5
14 Ng’ombe zetu na wachukue mizigo, Kusiwe na kushambuliwa. Wala kusiwe na kuhamishwa, Wala malalamiko katika njia zetu. 1 Samuel 13.17-13.23 Esaïe 24.11 Jérémie 14.2 Jérémie 13.17-13.19 Lamentations 1.4-1.6
15 Heri watu wenye hali hiyo, Heri watu wenye Bwana kuwa Mungu wao. Psaumes 33.12 Psaumes 146.5 Deutéronome 33.29 Psaumes 65.4 Ephésiens 1.3

Cette Bible est dans le domaine public.