1 Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana.
Psaumes 18.34 Psaumes 18.2 Psaumes 44.3-44.4 Ephésiens 6.10-6.11 2 Samuel 22.35
2 Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
Psaumes 18.2 Psaumes 91.2 Psaumes 59.9 2 Samuel 22.2-22.3 Psaumes 18.47
3 Ee Bwana, mtu ni kitu gani hata umjue? Na binadamu hata umwangalie?
Psaumes 8.4 Hébreux 2.6 Job 7.17 Psaumes 146.3-146.4 Job 15.14
4 Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
Psaumes 102.11 Psaumes 109.23 Job 8.9 Psaumes 62.9 Job 14.1-14.3
5 Bwana, uziinamishe mbingu zako, ushuke, Uiguse milima nayo itatoka moshi.
Psaumes 18.9 Psaumes 104.32 Hébreux 12.18 Exode 19.18 Esaïe 64.1-64.2
6 Utupe umeme, uwatawanye, Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
Deutéronome 32.23 Deutéronome 32.42 Psaumes 18.13-18.14 Psaumes 45.5 Psaumes 7.12-7.13
7 Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye, Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.
Psaumes 18.16 Psaumes 69.1-69.2 Apocalypse 17.15 2 Samuel 22.17 Psaumes 54.3
8 Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
Psaumes 12.2 Psaumes 41.6 Esaïe 44.20 Psaumes 62.4 Genèse 14.22
9 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.Psaumes 33.2-33.3 Psaumes 40.3 Psaumes 108.2-108.3 Psaumes 149.1 Psaumes 150.3-150.5
10 Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
Psaumes 18.50 Psaumes 140.7 Psaumes 33.16-33.18 2 Samuel 21.16-21.17 1 Samuel 17.45-17.46
11 Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
2 Samuel 16.5-16.14 2 Samuel 10.6-10.19 Psaumes 12.2 Psaumes 144.7-144.8 2 Samuel 17.1-17.14
12 Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
Psaumes 128.3 Psaumes 127.4-127.5 Job 42.15 Cantique 8.8-8.9 1 Pierre 3.3-3.6
13 Ghala zetu na zijae Zenye akiba za jinsi zote. Kondoo zetu na wazae Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.
Lévitique 26.5 Genèse 30.29-30.31 Lévitique 26.10 Psaumes 107.37-107.38 Deutéronome 28.4
14 Ng’ombe zetu na wachukue mizigo, Kusiwe na kushambuliwa. Wala kusiwe na kuhamishwa, Wala malalamiko katika njia zetu.
Lamentations 1.4-1.6 Zacharie 8.3-8.5 Deutéronome 28.7 Jérémie 14.18 Juges 5.8
15 Heri watu wenye hali hiyo, Heri watu wenye Bwana kuwa Mungu wao.
Psaumes 33.12 Psaumes 146.5 Deutéronome 33.29 Ephésiens 1.3 Psaumes 89.15