Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 39
Bible en Swahili de l’est


1 Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu. 1 Rois 2.4 Job 2.10 2 Rois 10.31 Psaumes 119.9 1 Chroniques 16.41
2 Nalikuwa sisemi, nalinyamaa kimya, Sina faraja, maumivu yangu yakazidi. Psaumes 38.13-38.14 Job 32.19-32.20 Esaïe 53.7 Matthieu 7.6 Matthieu 27.12-27.14
3 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka; Nalisema kwa ulimi wangu, Luc 24.32 Jérémie 20.9 Ezéchiel 3.14
4 Bwana, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani; Nijue jinsi nilivyo dhaifu. Psaumes 90.12 Psaumes 119.84 Psaumes 103.14 Job 14.13
5 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili. Psaumes 62.9 Psaumes 89.47 Psaumes 144.4 Job 14.1-14.2 2 Pierre 3.8
6 Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli; Hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili; Huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua. Luc 12.20-12.21 1 Corinthiens 7.31 Ecclésiaste 2.26 Ecclésiaste 5.14 Job 27.16-27.17
7 Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako. Psaumes 38.15 Psaumes 119.81 Romains 15.13 Psaumes 130.5-130.6 Psaumes 119.166
8 Uniokoe na maasi yangu yote, Usinifanye laumu ya mpumbavu. Psaumes 44.13 Psaumes 51.14 Psaumes 79.4 Joël 2.19 Romains 2.23-2.24
9 Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu, Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya. Job 2.10 2 Samuel 16.10 Daniel 4.35 Job 1.21 Lévitique 10.3
10 Uniondolee pigo lako; Kwa uadui wa mkono wako nimeangamia. Job 9.34 Job 13.21 Psaumes 38.3-38.4 Psaumes 32.4 1 Samuel 6.5
11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili. Job 13.28 Esaïe 50.9 Psaumes 102.10-102.11 1 Corinthiens 11.30-11.32 Psaumes 38.1-38.8
12 Ee Bwana, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote. 1 Pierre 2.11 Hébreux 11.13 Genèse 47.9 Psaumes 119.19 1 Chroniques 29.15
13 Uniachilie nikunjuke uso, Kabla sijaondoka nisiwepo tena. Job 10.20-10.21 Job 14.10-14.12 Genèse 42.36 Job 7.19 Job 14.5-14.6

Cette Bible est dans le domaine public.